BILLION 3.4 ZAKAMILISHA UJENZI HOSPITAL YA WILAYA YA LONGIDO, WANANCHI WAFURAHIA HUDUMA ZAKE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 8 November 2023

BILLION 3.4 ZAKAMILISHA UJENZI HOSPITAL YA WILAYA YA LONGIDO, WANANCHI WAFURAHIA HUDUMA ZAKE

 




Na Elinipa Lupembe, Longido


maipacarusha20@gmail.com


Serikali ya awamu ya sita imejenga Hospitali ya Wilaya ya Longido, kwa gharama ya shilingi Bilioni 3.4 , shilingi Bilioni 3 fedha kutoka serikali Kuu na milioni 500 fedha za mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19.


Aidha hospitali hiyo inategemea kuhudumia zaidi ya wagonjwa 175,915 wa wilaya ya Longido na wengine kutoka Nchi jirani ya Kenya, kukiwa na lengo la kutoa huduma zote za afya pamoja na kupunguza gharama kwa wagonjwa kusafiri mpaka Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha, sambamba na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo ya Rufaa.


Kiasi hicho cha fedha kimejumuisha ujenzi wa Jengo la Utawala, jengo la wagongwa wa nje OPD, jengo la Mionzi, jengo la wazazi, jengo la kufulia, jengo la dawa, wodi ya kina mama na wodi ya kinababa, maabara, jengo la kufulia na kichomea taka.



No comments: