JOWUTA yatoa maoni maboresho maslahi ya waandishi nchini - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 7 November 2023

JOWUTA yatoa maoni maboresho maslahi ya waandishi nchini

Katibu Mkuu wa chama Cha wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini Tanzania (JOWUTA) Selemani Msuya akimkabidhi maoni ya chama hicho mjumbe wa kamati ya kupokea maoni ya Hali ya uchumi Kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari, Sebastian Maganga, wengine kushoto ni naibu Katibu Mkuu wa JOWUTA, Said Mmanga, mjumbe wa bodi ya JOWUTA, Careen Tausi Mbowe na Kulia ni mtaalamu wa kamati hiyo, Dkt. Abdalah Katunzi

 



Na Mwandishi Wetu


maipacarusha20@gmail.com


Chama Cha wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini (JOWUTA) kimekabidhi maoni ya wanachama wake katika Kamati ya kupokea maoni juu ya Hali ya Uchumi kwa vyombo vya habari ambayo iliteuliwa na Waziri wa Habari Mawasiliano na teknolojia ya Habari,Nape Nnauye.


Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando ,imekuwa ikipokea maoni toka kwa wadau mbalimbali jinsi ya kuondoa changamoto na Hali ya uchumi katika vyombo vya habari nchini.


Katibu Mkuu wa chama Cha wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini Tanzania (JOWUTA) Selemani Msuya  amekabidhi maoni ya chama hicho Leo November 7 kwa Wajumbe wa Kamati hiyo.


 Maoni ya JOWUTA yamepokelewa na mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo, Sebastian Maganga, ambaye alikuwa ameambatana na Mtaalam wa Kamati hiyo, Dk Abdalah Katunzi.


Viongozi wengine wa JOWUTA ambao walishiriki kuwasilisha maoni ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa JOWUTA Said Mmanga na mjumbe wa bodi ya JOWUTA, Careen Tausi Mbowe .


JOWUTA ndio chama pekee cha wafanyakazi kisheria ambacho kinaundwa na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kikilenga kukabiliana na changamoto za malipo duni ya wanahabari, kutokuwa na mikataba ya Kazi , kuachishwa kazi kinyume cha sheria na kutolipwa stahiki zao.



No comments: