RC MONGELLA ARIDHISHWA NA MRADI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI SINYA; WANANCHI WAMSHUKURU MAMA SAMIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 9 November 2023

RC MONGELLA ARIDHISHWA NA MRADI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI SINYA; WANANCHI WAMSHUKURU MAMA SAMIA

 







Na Elinipa Lupembe, Longido 


maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella, ameridhishwa na  utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Sinya, mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama shilingi milioni 470 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mpango wa Kuboresha Miundombinu ya Serikali nchini (SEQUIP) shule ambayo imesajiliwa kwa namba SINYA S. 6298.


Mhe. Mongella ameonesha kuridhishwa na mradi huo, mara baada ya kutembelea na kukagua hali halisi na muonekana wa majengo yaliyokamilika kwa viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali.


Katika mradi huo ameupongeza uongozi wa wilaya ya Longido, viongozi wa chama, baraza la Madiwani pamoja na Mwalimu msimamizi wa mradi huo ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari Tingatinga kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi pamoja na kufanikisha usajili wa shule hiyo ambayo inatarajia kupokea wanafunzi mapema Januari 2024.


Aidha amewataka viongozi na watalam kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika na kuhakikisha miradi ya maendeleo inasimamiwa vema na kukamilika kwa wakati ili iweze kutoa huduma kwa wananchi.


"Miradi hii ya elimu inaposhindwa kukamilika kwa wakati, tunawakosea haki watoto wetu, serikali imetoa fedha za kukamilisha miradi, jukumu lenu ni kusimamia ili ikamilike kwa wakati na watoto wapate haki yao ya msingi".Amesema Mhe. Mongella.


Hata hivyo wananchi wa kata ya Sinya, wameishukuru serikali kwa ujenzi wa shule hiyo mpya, shule ambayo licha ya kukata kiu yao ya muda mrefu, itawapa fursa watoto wao kusoma karibu na nyumbani.


Mwenyekiti wa UWT kata ya Sinya, Norkishumu Otuma Sakita, amesema kuwa licha ya kuwa tulitamani kuwa na shule ya sekondari lakini hatukuwahi kuwaza kuwa na shule kama tutapata shule mapema, mama Samia ametukumbuka sisi wamama, watoto watapata elimu ya sekodnari na kwenda chuo kikuu kama watoto wengine.


Naye Nangakiwa Gwarugulito, amemshukuru Rais, mama Samia kwa kuwajengea shule kijijini kwao, walikuwa na shule ya msingi tu, walitumia gharama kubwa kuwapelekea watoto shule za mbali, lakini sasa wamepata shule  nyumbani.


 "Tunaamini kwa sasa watoto wetu watapata nafasi ya kusoma chuo kikuu, watoto wetu watakuwa wasomi na kuwa viongozi wa kubwa wa nchi hii, kijiji chetu kitakuwa na  wasomi sasa" Amesema Nangakiwa


Akiwasilisha Taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule sekondari Tingatinga Mwl. Pantaleo Pareso amesema kuwa, milioni 470 zimejenga vyumba 8 vya madarasa, jengo la utawala, jengo la Maabara, chumba cha TEHAMA, matundu 16 ya vyoo, ununuzi wa matank ya kuhifadhia lita 1000 za maji







No comments: