LINDI MWAMBAO WAUZA TANI 1,324 ZA KOROSHO KWA BEI YA JUU TSH.2,460/= KWA 2,360/= - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 23 November 2024

LINDI MWAMBAO WAUZA TANI 1,324 ZA KOROSHO KWA BEI YA JUU TSH.2,460/= KWA 2,360/=

 




Na Mwandishi Wetu, Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Chama Kikuu cha Ushirika LINDI MWAMBAO, kimeuza Korosho za Wakuli kwa bei ya juu Tsh.2,460/= na 2,360 Bei ya chini katika mnada uliofanyika leo tarehe 23 Novemba 2024.


Mnada huo ambao umeendeshwa na Soko la bidhaa Tanzania TMX, umefanyika katika ofisi ya Chama cha Msingi Nyangao Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi.


Akitoa salamu kwa wakulima, Bi.Consolata Kiruma ambaye ni Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, ameelezea mafanikio ya TMX katika minada ya msimu 2024/2025 hali ambayo yamepelekea wakulima kushuhudia minada kwa njia ya mtandao tofauti na miaka iliyopita ambayo wanunuzi walikuwa wanalzimika kufika mnadani.


"Tuko kwenye ziara ya kuangalia mwenendo wa ufanisi wa mauzo ya korosho kupitia mfumo wa TMX na tumejionea namna ambavyo wakulima wamenufaika na wenyewe wamekiri juu ya hilo.


Naye Abel Mtembeli kutoka Wizara ya Kilimo, ameelezea dhamira ya serikali katika kuendelea kukuza mauzo ya nje ambayo yatachangiwa na mifumo mizuri ya uuzaji kama TMX, na kuwasisitiza wakula kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili malengo ya serikali yaweze kutimia.


Mwenyekiti wa Lindi Mwambao Hassan Mohamed Mnumbe amesema kuwa wakulima wameridhia kuuza Korosho hizo baada ya kujiridhisha kufuatia bei iliyotajwa na wanunuzi wakati wa mnada.

No comments: