WAZAZI WATAKIWA KUSIMAMIA ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 29 May 2023

WAZAZI WATAKIWA KUSIMAMIA ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA

 




NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC RUFIJI



MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Rufiji Ally Maliti amewataka wazazi kuacha kuwa kikwazo cha kukatisha masomo na ndoto za Watoto wa kike na kiume badala yake kuhakikisha wanasimamia maswala ya Elimu na Malezi Ili kuleta tija katika kusaidia kupunguza changamoto za kielimu na maadili katika kijami.

Ameyasema hayo katika kikao na viongozi pamoja na wanajumuiya ya Wazazi Kata ya Mbwara ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Kata Kwa Kata kutembelea jumuiya za Wazazi chama Cha mapinduzi Wilayani Rufiji.

" Tumepokea taarifa kuhusiana na Watoto wanaopata ujauzito wakiwa shuleni wengi wao chanzo ni sisi wazazi na hii ni hatari kubwa ni lazima kubadilika tusikatishe ndoto za Watoto wetu tuna kazi kubwa ya kusimamia Elimu, na Malezi" amesema Mwenyekiti.

Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Serikali Diwani wa Mbwara Juma Ligomba ameipongeza Serikali Kwa kutoa fedha za utekelezaji wa Miradi zaidi ya shilingi Bilioni Moja Kwa Kata hiyo.

Aidha amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utelii Mohamed Mchengerwa kwa namna ambavyo anajitoa kupigania Maendeleo ya Wilaya ya Rufiji hususani Kata ya Mbwara ambayo Ilikuwa ikikabiliwa na vikwazo vingi ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo hadi Sasa zaidi ya kilometa nane tayari zimefanyiwa matengenezo na barabara kupitika kwaurahisi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wazazi Taifa Fatima Msumi amewataka Wazazi kuzungumzia maswala ya malezi na jinsia kwa Watoto hususani vikwazo katika  mmonyoko wa maadili ikiwemo madhara ya mahusiano ya jinsia Moja Kwa Watoto wa kiume na wa kike.

" Tusikae kimya kwa kufikiri kuwa changamoto hizi ni za nje ya Wilaya yetu hata kwetu zipo. Tuzngumze na kuwalinda Watoto wetu." alisisitiza Bi. Fatum

Katika hatua nyingine Jumuiya hiyo imetoa kadi Kwa Wanajumuiya 1300 pamoja na kutembelea Wagonjwa Hospital ya Wilaya, kituo Cha Afya Mohoro na kutoa misaada na zawadi ikiwa ni pamoja na Baskeli Moja ya walemavu, sabuni za maji, unga na Sukari pamoja na taulo za kike kwa Watoto wa kike Shule ya Msingi Mohoro na Shule ya Sekondari Utete, Mkongo na Mwaseni Wilayani Rufiji.

No comments: