MIILI 25 WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI JIJINI ARUSHA YAAGWA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 27 February 2024

MIILI 25 WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI JIJINI ARUSHA YAAGWA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID

 


Miili ya waliofariki ikishushwa Toka katika magari tayari Kwa kuagwa na wakazi wa Arusha


Na :Andrea Ngobole, MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


Miili ya watu 25 waliofariki kwa ajali iliyohisisha Lori lililobea mtambo wa kuchongea barabara na magari mengine matatu, inaagwa Leo February 27 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


Ajali hiyo ilitokea February 24 majira ya jioni eneo la Ngaramtoni kibaoni Bypass Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela atakayeongoza wakazi wa Mkoa wa Arusha kuaga miili hiyo amesema kuwepo Kwa Zoezi Hilo hakuwezi kuathiri maandamano ya Chadema yanayofanyika mkoani Arusha leo kwani  Serikali inatambua maandamano hayo.


"Naomba isije ikapotoshwa si kwamba hatutambui uwepo wa maandamano, ratiba ya maandamano IPO na IPO kisheriana mifumo yote ya Serikali itahakikisha maandamano haya yanakuwa salama kama yalivuosimamiwa Maneno mengine" alisema Mongela


Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha shughuli za kuaga miili hiyo itaanza saa tatu asubuhi na kukamilika saa Tano Kisha miili hiyo kusafirishwa maeneo mbalimbali Kwa ajili ya maziko

No comments: