Dkt Samia: Tunahitaji mfumo wa ufuatiliaji wafungwa wanaotoka gerezani - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 9 May 2026

Dkt Samia: Tunahitaji mfumo wa ufuatiliaji wafungwa wanaotoka gerezani





Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametaka kuwepo mfumo wa ufuatiliaji wa wafungwa wanaomaliza vifungo vyao, ili kujua walipo na wanachofanya. 


Amesema mfumo huo, utasaidia pia kuwaunganisha na taasisi za uwezeshaji na sekta binafsi inayoweza kuwatumia katika shughuli mbalimbali wakajiingizia kipato na kuacha kurudia uhalifu.


Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi Mei 9, 2026 wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi ngazi ya juu Kodi namba 48 kwa mwaka 2025/26 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania.


Ametaka pia ifanywe tathmini kujua kiwango cha wanaorudia uhalifu baada ya kumaliza kifungo 


Amesema takwimu hizo zitasaidia kupima na kujua iwapo urekebishaji unaofanywa unafikia malengo na matarajio au kuna mapungufu na yarekebishwe.


"Nataka kuwa na mfumo madhubuti wa ufuatiliaji na tathmini baada ya kumaliza vifungo," amesema.

No comments: