VIONGOZI WA NGORONGORO NA KARATU WAJADILI UVAMIZI WANYAMAPORI KATIKA MAKAZI YA WATU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 20 June 2023

VIONGOZI WA NGORONGORO NA KARATU WAJADILI UVAMIZI WANYAMAPORI KATIKA MAKAZI YA WATU

 



Sophia Fundi,Karatu

maipacarusha20@gmail.com


Kutokana na changamoto ya wanyama wanaovamia makazi ya wananchi walioko  pembezoni mwa msitu wa Ngorongoro wilayani KARATU, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo wamekutana  na uongozi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kujadili changamoto hiyo.


Katika majadiliano hayo pande hizo mbili wameweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na wanyama hao ambapo wamepanga kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kukabiliana nao.


Sambamba na elimu pia wamejiwekea mikakati ya kuweka uzio maeneo ambayo yameathirika pamoja na kuweka mizinga ya nyuki ili kuwafukuza wanyama kama Tembo ambao wamekuwa wakiwajeruhi wananchi na kuwaua na pia kuharibu mazao yao.


Akizungumza katika mjadala huo naibu kamishna wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Elibariki Bajuta alisema kuwa mamlaka imejipanga kuweka uzio kilometa 30 katika maeneo yaliyoathiriwa na wanyama kuhakikisha wananchi walioko pembezoni mwa msitu wanakuwa huru kufanya shughuli zao za kijamii.



Alisema kuwa watashirikiana na halmashauri ya wilaya ya KARATU kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kuhakikisha maeneo yote yanapata ulinzi wa kutosha kuwazuia wanyama wakali ambao wanatoka msituni.


Pia katika mjadala huo pande hizo mbili zilijadili ni kwa namna gani wanaboresha huduma kwa wageni (watalii)kutokana na idadi kubwa katika kipindi hichi.


Akizungumza katika mjadala huo mkuu wa wilaya ya Karatu Dadi Kolimba alisema kuwa asilimia 80 ya wageni wanaoigia ndani ya Kreta na Serengeti wanapitia Katika wilaya ya Karatu hivyo ni fursa kwa wadau wa utalii na wananchi wa Karatu kuwekeza wilayani hapo.


Aliwataka wadau wa utalii kwenye hoteli zao kuboresha huduma ikiwemo kwa wageni ikiwemo kuongeza vitanda kwani kutokana na filamu ya  Royal Tower aliyotangaza Dkt  Samia Suluh Hasan wanategemea kupata wageni wengi Sana.


"Katika kipindi hichi wageni watakuwa wengi Sana naomba wawekezaji waje kuwekeza Karatu na walio na mahoteli waongeze huduma ikiwemo vitanda vya kutosha"alisema Kolimba.



No comments: