Handsome Boy Auliwa na msichana kwa kugoma kulipa" luku" ya 1000 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 20 June 2023

Handsome Boy Auliwa na msichana kwa kugoma kulipa" luku" ya 1000

 




Erick Adam, enzi za Uhai wake

Mwandishi wetu, Arusha 

maipacarusha20@gmail.com


Jeshi la polisi mkoa Arusha, linamshikia msichana Brandina Fred  kwa tuhuma za kumuuwa Mpangaji mwenzake Erick Adam, mkazi wa kijiji cha IIkirev ,Kata ya Olturoto   wilayani Arumeru


Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amesema tukio hilo lilitokea majira ya mchana wakati, Blandina akiwa na kisu akijiandaa na kupika.


"Kilichotokea  ni kuwa wote ni wapangaji walikuwa wakigombana huyu binti alikuwa na kisu kwa kuwa alikuwa jikoni, sasa ndio alimchoma mwenzake"amesema


Amesema Adam alifariki  kutokana na kutokwa na damu nyingi b baada ya kuchomwa kisu.


Kamanda Masejo amesema, Jeshi hilo bado linamshikilia kwa mahojiano, mtuhumiwa huyo na bado anahojiwa kuhusiana na tuhuma hizo.

"Taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani kutokana na tuhuma ambazo zinamkabili" alisema kamanda Masejo


Mwili wa Adam umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mountmeru kwa uchunguzi zaidi.


No comments: