BITEKO: MGAO WA UMEME UKO UKINGONI KUISHA, AONYA WANANCHI WANAOCHEPUSHA MITO YA MAJI INAYOKWENDA KWENYE MABWAWA YA UMEME - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 24 February 2024

BITEKO: MGAO WA UMEME UKO UKINGONI KUISHA, AONYA WANANCHI WANAOCHEPUSHA MITO YA MAJI INAYOKWENDA KWENYE MABWAWA YA UMEME

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ametoa onyo kali kwa baadhi ya wananchi wenye tabia ya kuchepusha mito ya maji inayokwenda kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme kwa shughuli zao binafsi  pamoja na kufanya shughuli za kilimo katika vyanzo vya maji, vitendo vinavyoharibu vyanzo hivyo vya maji.


Naibu Waziri mkuu huyo pia amesema Mgao wa Umeme upo ukingoni kuisha kwa kuwa Serikali imeshafanya jitihada kubwa ya kukabiliana na changamoto ya Umeme ikiwa ni pamoja na kuwekeza fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya Umeme.


Dkt. Biteko ameyasema hayo Februari 23 ,2024 alipoambatana na Waziri wa maji Juma Aweso kwenye ziara ya kukagua Bwawa la kuzalisha Umeme la Kidatu.


“Hatutawafumbia macho watu wanaoharibu vyanzo vya maji, kwani unasababisha ukame katika mabwawa haya na lawama zinaishia kwa Tanesco na Serikali, hivyo tutunze vyanzo vyetu vya maji,”amesema Dk Biteko


“Serikali hii ya Awamu ya sita ya Dkt. Samiah Suluhu Hassan imeshatoa fedha nyingi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya Umeme nchini, niwaombe wananchi kuwa wavumilivu kidogo, suala la mgao wa Umeme linakwenda kwisha,!"amesema Dk Biteko



Amewataka watanzania kuwa wavumilivu kidogo changamoto ya umeme ambayo inakwenda kuisha.


Aidha Dk Biteko ameridhishwa na kiwango cha maji kilichopo katika Bwawa la Kidatu,maji ambayo pia yatatumika kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere, kupitia mikondo ya maji ya mto ruaha mpaka kufika mto Rufiji.


Aidha ameitaka menejimenti ya  shirika la umeme Tanesco kuwaondoa kwenye mgao wananchi wanaoishi kandokando ya vyanzo vya kuzalisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini.


Pia ameonya maafisa wa Tanesco wanao wasumbua wateja na kupiga marufuku mapumziko ya likizo kwa watumushi wote wa Shirika hilo wakati huu wa changamoto ya umeme, sambamba na kuahidi kuunda timu maalumu ya wataalam wa kisekta kushughulikia changamoto ya umeme.


Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Awessu, ameahidi kushirikiana na wizara ya Nishati katika kutokomeza ukame,katika mabwawa ya kuzalisha Umeme, lakini pia katika kuhakikisha maji yanapatikana kwa wananchi wote kwani Umeme na maji ni sekta zinazotegemeana.


Aweso ameahidi kuwa Wizara yake itahakikisha inalinda vyanzo vya maji na kuwaonya viongozi na watendaji kuacha kuzoea shida za wananchi.



No comments: