MLIMA KIDENGE SAME WATARAJIA KUINGIA KWENYE ORODHA YA VIVUTIO VYA UTALII - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 24 February 2024

MLIMA KIDENGE SAME WATARAJIA KUINGIA KWENYE ORODHA YA VIVUTIO VYA UTALII

 

Mlima Kidenge uliopo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro



Na: Lilian Kasenene, Same


maipacarusha20@gmail.com


Mlima Kidenge uliopo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro unatarajiwa kuingizwa katika orodha ya vivutio vya utalii vilivyopo kwenye wilaya hiyo baada ya kuonekana kuwavutia watalii wazawa waliotembelea eneo hilo.


Tamasha la kuibua na kutangaza vivutio vya utalii Wilaya ya Same 'Same Utalii Festival' tumeanza na tamasha la kwanza kufanyika katika Wilaya hiyo.


Mamia ya watalii kutoka ndani na nje ya wilaya ya Same wametambelea Mlima huo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya, kupanda kilele cha mlima huo unaotajwa kuwa wa kipekee kulingana na mandhari yake.


“Mama yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani alianza kwa kutuonesha njia ya nini tunachopashwa kufanya na leo kupitia wilaya ya Same nimeandika historia kwenye maisha yangu kwa  kupanda Mlima Kidenge kipindi tunapanda tulikua tunasikia Joto,Jasho  lakini tulipofika kileleni Upepo wa beach (Ufukwe wa bahari) unasubiri”.Amesema mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya.




Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema wazo la kuanzisha tamasha hilo kuibua maeneo yenye vivutio ambayo hayajatangazwa ni matokeo ya ziara ya mafunzo waliyofanya baadhi ya wakuu wa Wilaya Nchini China, ambapo pamoja na mambo mengine walijifunza uzoefu wa kinacho fanyika nchini humo kuibua vyanzo vya mapato.


“Tulienda kwenye mafunzo Nchini China kujifunza mambo mbalimbali ya maendeleo na kujionea wanavyo fanya wenzetu kujiletea maendeleo ambapo nikiwa kule kuna sehemu tulipita tukaona mlima unaofanana kabisa na Mlima Kidenge uliopo kwenye wilaya yetu ya Same tofauti yake Mlima ule ulikua wa Kutengenezwa na huu wa kwetu ni mlima asilia hivyo nikaona nikirudi jambo la kwanza ni kuangalia uwezekano wa kugeuza mlima huu kuwa fursa kwenye utalii,”.amesema mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni.


Amesema malengo ya tamasha hilo la Same Utalii Festival ni kuibua vivutio ambavyo havijatangazwa viweze kufahamika, pia kuviendeleza viweze kuwa sehemu ya mapato kwa kuwezesha watalii wakiwemo wazawa na raia wa kigeni kutembelea maeneo hayo ambayo katika wilaya ya Same pekee yapo mengi.


Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Same walioshiriki kwa kupanda mlima huo wamesema ni vema kukafanyika utafiti utakao shirikisha wakazi kwenye kila eneo kuainisha vivutio vilivyopo kwenye maeneo yao ikizingatiwa mkazo kwenye kuhamasisha watalii unaelekezwa zaidi kwenye maeneo ambayo tayari yanafahamika.




No comments: