![]() |
| Dkt Noel Mpeta akimtibu mgonjwa wa macho Asheri Musa wakati wa matibabu yaliyotolewa na Mo Dewji Foundation yaliyofanyika katika Hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba Mkoa wa Singida |
SELF TAKAZA – IRAMBA
maipacarusha20@gmail.com
WANANCHI Wilayani Iramba, Mkoani Singida Wameipongeza na Kuishukuru taasisi ya Mo Dewji Foundation kwa kutoa msaada wa matibabu ya Macho na Saratani ya Shingo ya mlango wa Kizazi Na Saratani Ya Matiti kwa Wanawake.
Pongezi na shukrani hizo zimetolewa juzi na wagonjwa waliopatiwa huduma katika Hospitali ya Wilaya Kiomboi ambapo wagonjwa walisifia huduma waliopata na wengine kupewa miwani ya kusomea bila malipo.
Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi Dkt James John Komanya kuwa amepokea wataalam wa magonjwa ya macho, saratani ya shingo ya mlango wa kizazi, pamoja na saratani ya matiti kwa wanawake. Hata hivyo Dkt Komanya amesema wataalam wamefanya kazi hiyo kuanzia tarehe 27/03/2026 hadi 30/03/2026.
“Naishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira mazuri ya matibabu kwa jamii na kuchangia kiasi kidogo cha fedha ambapo hivi karibuni madaktari bigwa na wabobezi wa magonjwa mbalimbali walifanya kazi ya kutibu katika Hospitali hii na leo hii tumepata madaktari toka MO Dewji Foundation.
Hivyo tunaomba Taasisi zingine ziige mfano huu, wataalam hawa wa MO Dewji wametibu wagonjwa 4191 wa macho, 1167 saratanin ya matiti, na 997 wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi “Alisema Dkt Komanya
Kwa upande wake Mratibu wa MO Dewji Foundation toka Dar es salaam Kolnel Matheo amesema kuwa Taasisi hiyo inatoa matibabu bure ili iweze kusaidia jamii
“Saratani ya shingo ya mlango wa kizazi na saratani ya matitit ni magonjwa hatari sana usipowahi kuyafanyia uchunguzi. Hivyo inawapata watoto wa kike wenye umri wa miaka 11, wapatiwe chanjo mapema ili kuepuka na ugonjwa huo hatari: Alitilia mkazo Dkt huyo
Kwa upande wa Daktari wa macho Dkt Salim Mohamed alisema amewafanyia matibabu ya macho kwa kutoa miwani ya kusomea kwa wanao stahili.
“Nijukumu la kila mtu kuhakikisha analinda macho yake kwani kwa maisha ya sasa watu wengi hutumia simu, runinga na kompyuta. Changamoto nyingine ni kuhusu vumbi kutosafisha macho inavyostahili, hivyo nasisitiza jamii kuwa makini”, alisema Dkt Salim
Naye bibi Winjuma Andrea Nangali aliyepata matibabu ya macho amesema wananchi waliokwenda kupata matibabu wanamshukuru sana MOHAMED DEWJI kwa kubuni huduma ambayo mtu wengi hushindwa kumudu gharama ya matibabu.
“Huyu MOHAMED DEWJI ni mtu mzuri ambaye anajali sana afya za Watanzania nashindwa nisemeje bali namuombea kwa mwenyezi Mungu ampe uwezo wa kutosha ili wananchi wapate matibabu kama taasisi yake inavyotoa huduma hata hivyo pamoja nakutoa huduma anatoa chakula kwa wagonjwa wake waliokwenda kupata matibabu ambayo ni bure na chakula bure huu ni ubinadamu uliopitiliza, Mungu ampe umri mrefu” Alisema mama Nangali
Hali kadhalika diwani wa kata ya Kiomboi Diwani Omari Hassan amesema MOHAMED DEWJI amefanya kitendo cha kiungwana na cha kumpendeza Mwenyeezi Mungu.
“Mimi sikuwepo Hospitali lakini wananchi wangu waliokwenda kupata tiba wamesifia Madaktari na Wahudumu walivyokua mahiri na wakarimu, natoa wito kwa wananchi zinapojitokeza fursa kama hizi wajitokeze kwa wingi” Alisisitiza Diwani Omari
MWISHO


No comments:
Post a Comment