VIJANA Vyuo Vikuu Wahamasisha Uzalendo - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations

Saturday, 16 May 2026

VIJANA Vyuo Vikuu Wahamasisha Uzalendo

Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Geofrey Kiliba amesema wanavyuo wa mkoa wa Dar es Salaam wanaunga mkono tamko 'never again' lililotolewa na vijana Mkoa wa Dodoma mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kiliba ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Mei 16, 2026 Jumamosi katika kongamano la wanafunzi wa vyuo lenye kauli mbiu 'never again' tuipende, tuitunze , tuilinde nchi yetu' lililofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na TAHLISO mkoani hapa.

Msingi wa kauli ya Kiliba aliuejenga wakati akieleza madhumuni mahususi ya kongamano hilo huku akirejea ujumbe vijana wa Dodoma waliotoa mbele ya Dkt Samia kwamba hawako tayari kushirikiana na mtu yeyote anayetaka kuvunja misingi ya amani na mshikamano uliopo huku wakisisitiza yaliyotokea Oktoba 29 yasijirudie tena.

Maelfu ya wanafunzi kutoka vyuo na vyuo vikuu mbalimbali nchini wakiwa kwenye maandamano wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe za kuhamaisha amani na uzalendo wakati wa uzinduzi wa Kongamano la ‘Never Again’ lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO)  leo Mei 16,2026 jijini Dar es Salaam. Maandamano hayo yalianzia katika Kiwanja cha Kinesi hadi Ubungo Plaza.
Viongozi wa Serikali akiongozwa na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Vijana, Joel Nanauka, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Wakili Albert Msando na viongozi wa Serikali za wanafunzi na wanafunzi wakiwa kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza leo Mei 16,2026 tayari kwa kuanza Kongamano la Wanafunzi la ‘Never Again’ lenye kauli mbiu inayosema ‘Tuipende, Tuitunze, Tuilinde nchi yetu’.

No comments: