MAGARI YANAYOTUMIA MFUMO WA UMEME SULUHISHO LA UTUNZAJI MAZINGIRA NA UHIFADHI NCHINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 28 February 2023

MAGARI YANAYOTUMIA MFUMO WA UMEME SULUHISHO LA UTUNZAJI MAZINGIRA NA UHIFADHI NCHINI



mkurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul na Emotion Afrika,Satbir Hanspaul akiwaonesha wajasiriamali magari ambayo wamefunga mfumo wa umeme badala ya mafuta ya dezeli ama petroli  baada wajasiriamali hao kupitia taasisi ya SEED Tanzania,kutembelea kiwanda chake


Mkurugenzi wa Kampuni ya Hanspaul na Emotion Afrika,Satbir Hanspaul akiwaonesha wajasiriamali magari ambayo wamefunga mfumo wa umeme badala ya mafuta ya dezeli ama petroli  baada wajasiriamali hao kupitia taasisi ya SEED Tanzania,kutembelea kiwanda chake

Mmoja wa madereva wa magari ya utali akiwa porini na gari linalotumia diesel ila pia limefungwa umeme wa jua kwa ajili ya kuchaji vifaa vya umeme na kuwasha taa zaidi ya kumi wawapo porini




NA: MWANDISHI WETU, MAIPAC



maipacarusha20@gmail.com


Wamiliki wa magari ya Utalii nchini, wameshauriwa kuanza kutumia magari yanayotumia umeme badala ya mafuta, ili kuunga mkono jitihada za dunia kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ambao unachangia mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kukabiliana na bei kubwa za mafuta .

Magari ya umeme hayatumii mafuta na gharama ni kufungwa mfumo wa umeme kwa magari ya Utalii ni Dola kati ya 50 hadi 85 na mtumiaji atakuwa akiongeza umeme kwenye betri ya gari tu.

Magari haya pia ni suluhu ya ajali kwani mtumiaji anauwezo wa kujipangia mwendo Kasi barabarani na kuweka kikomo cha mwendo Kasi ambapo gari kuweza kusafari umbali mrefu kama gari za mafuta kulingana na umeme wa gari.

Mkurugenzi wa kampuni za Hanspaul , Satbir Hanspaul akizungumza katika mkutano wa wajasiriamali kukuza ubunifu na uthubutu katika biashara ambao, uliandaliwa na taasisi ya CEED-Tanzania ,Hanspaul alisema ni wakati muafaka sasa kwa kuanzia sekta ya utalii kufanya utalii ulio salama kwa mazingira.

Alisema matumizi ya magari ya umeme ambayo gharama za uendeshaji wake ni kidogo kuliko mafuta, yatasaidia sana kutangaza Utalii wa Tanzania, kipindi hiki ambacho Rais Samia Suluhu amezindua filamu ya Royal Tour kwani mazingira ya hifadhi yatakuwa mazuri na kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ambayo inachangia athari ya mabadiliko ya tabia nchi duniani.

Hanspaul alisema wakati dunia kwa sasa imelenga ifikapo mwaka 2030 hadi 2050 iwe imepunguza kiasi kikubwa matumizi ya mafuta katika uendeshaji wa magari na viwanda ni bora kuanza sasa kubadili mfumo wa magari .

"Sisi tumeamua kuanzisha kampuni ya E- Motion Afrika ambayo itajikita katika kubadilisha magari kutoka katika matumizi ya mafuta kwenda kutumia umeme na baadae gesi na tayari hadi sasa tangu kuanza mradi huu mwaka 2018 magari 20 ya utalii yanatoa huduma katika hifadhi vizuri baada ya kujiridhisha katika utendaji kazi wake"alisema

Alisema kiwanda hicho, kinauwezo wa kubadili mfumo wa magari kutoka mafuta hadi umeme hadi magari 800 kwa mwaka lakini bado wamiliki wengi wa magari hawajajitokeza kupata huduma hiyo.

Hanspaul alisema ili kuhakikisha huduma ya magari ya umeme, inapatikana kwa urahisi tayari wamekuwa na makubaliano na shirika la ugavi wa umeme(TANESCO) kwa kushirikiana na wadau wengine,ikiwepo shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) kuwa na vituo kadhaa vya kujaza umeme magari.

"tayari tunamakubaliana mazuri na serikali na ifikapo mwezi desemba tutaanza kuwa na vituo vya kujaza umeme kama ilivyo vituo vya magari kwani Tanzania kwa sasa tuna umeme wa kutosha"alisema

Alisema wameamua kuanza kubadili mfumo wa magari ya utalii na baadaye magari ya ainba zote yatakuwa yakipata huduma hiyo na yatalazimika kuongezwa ukubwa wa bodi ili kupata nafasi ya kuwekwa betri za kuongeza umeme.


Akizungumzia ubunifu huo, Mkurugenzi wa taasisi ya CEED- Tanzania, Atiba Amalile aliwataka wafanyabiashara sekta ya utalii na wengine kutumia huduma ya kubadilisha magari kuwa ya umeme ili kuonesaha dunia kuwa Tanzania tumeanza kutekeleza makubaliano ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.


Alisema kilichofanyika katika kampuni ya Hanspaul ni kuthubutu kufanya ubunifu jambo ambalo linapaswa kuigwa na wafanyabiashara na wajasiriamali wengine hapa nchini, ili kukuza biashara zao na mitaji.


"lengo la kuwakutanisha wajasiriamali hawa na Satbir leo ni kupata uzoefu juu ya ubunifu wake kwani ni mmoja wa vijana wawekezaji wazawa wenye mafanikio kutokana na kuongoza vizuri makampuni matano"alisema


Mkurugenzi wa kampuni ya Afrika bound Tours (T) Ltd Ambrose Mtui licha ya kupongeza ubunifu wa Hanspaul aliishauri kuwepo vituo vya kuongeza umeme barabarani ili wanunuzi wa magari wasiwe na hofu ya kupata umeme wakiwa na watalii.


"kama kukiwa na vituo vingi vya kutoa umeme wa magari itakuwa jambo zuri kwani tayari watalii wengi wanapenda kupanda magari ambayo yanatumia umeme badala ya mafuta kutokana na kuwa rafiki wa mazingira lakini wanaona wanyama kwa urahisi kwani hayana sauti wala moshi"alisema.


No comments: