![]() |
Baadhi ya walimu wilayani Karatu waliojitoa CWT |
![]() |
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Karatu |
NA: SOPHIA FUNDI KARATU.
maipacarusha20@gmail.com
Madiwani halmashauri ya wilaya ya KARATU mkoani Arusha wameridhia kwa pamoja ombi la waalimu zaidi ya 500 ya kutokatwa mishahara yao na kilichokuwa chama Cha waalimu CWT baada ya waalimu hao kujitoa na chama hicho na kujiunga na chama kipya CHAKUHAWATA.
Ombi Hilo limewasilishwa na katibu msaidizi wa chama hicho bw Deogratius Mmao akifuatana na baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao walilaani kitendo Cha idara ya utumushi kuendelea kukata mishahara yao nakuelekeza CWT Jambo ambalo litaleta mgogoro baina yao.
Madiwani hao wakichangia hoja kwa pamoja waliunga mkono hoja na kumtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Juma Hokororo kupitia idara ya utumishi kuheshimu hoja ya waalimu hao na kuacha kuwakata mishahara yao nakuelekeza CWT badala yake waelekeze kwenye chama kipya.
Walimwagiza mkurugenzi mtendaji bw Hokororo kupitia idara ya utumishi kuanzia mwezi huu wa nane 2023 kuhakikisha hakuna mshahara wa mwalimu unaokatwa na chama hicho ili kuheshimu uhuru wa mwalimu na kuepuka migogoro baina ya halmashauri na waalimu.
"Mkurugenzi tunakuagiza hakikisha hakuna mshahara wa mwaalimu unaokatwa na chama hicho kuanzia mwezi huu wa nane ni uhuru wa mwalimu kujiunga na chama anachokipenda tuwaache wachague wenyewe tusiwalazimishe, hatutaki kuingia kwenye migogoro na waalimu" alisema John Lucian.
Akizungumza na wanahabari kaimu katibu wa chama hicho Mmao alisema kuwa waalimu hao wamefuata taratibu zote za utumishi na kujiunga na chama hicho kipya CHAKUHAWATA.
Kwa upande wake Mwenyekiti msaidizi wa CHAKUHAWATA bw Festo Mbilinyi ameshukuru Baraza la madiwani kwa kupokea ombi lao na kukubaliwa ambapo aliomba mchakato huo uharakishwe ili uweze kuingia kwenye utekelezaji.
No comments:
Post a Comment