MAMLAKA UVUVI BAHARI KUU KUJENGA KIWANDA CHA KUCHAKATA SAMAKI JIJINI TANGA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 9 February 2023

MAMLAKA UVUVI BAHARI KUU KUJENGA KIWANDA CHA KUCHAKATA SAMAKI JIJINI TANGA

 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya kusimamaia uvuvi na Bahari kuu Tanzania Emanuel Sweke akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma


Wandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu wa usimamizi wa uvuvi wa Bahari kuu Tanzania pichani hayupo

NA: SHAKILA NYERERE, DODOMA

maipacarusha20@gmail.com


 MAMLAKA ya kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu imesema kuwa katika kutekeleza mikakati yake inatarajia Kujenga Kiwanda kikubwa Cha kuchakata Samaki Mkoani Tanga ambacho kitakuwa na uwezo wakuzalisha Tani zaidi ya 100 kwa siku ambacho kitagharimu Dola Milioni10 na kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania.


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Emanuel Sweke amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya usimamizi wa Bahari Kuu.


Aidha katika kudhibiti uvuvi haramu Mamlaka hiyo imeweza kuweka mifumo madhubuti ambayo inaendana na Teknolojia kwakufanya doria mbalimbali kwajili ya kukomesha suala la uvuvi haramu.

 Amesema Mamlaka hiyo imeweza kuvunja rekodi ya kukusanya Mapato mengi kwa Kipindi Cha 2022 hadi kufikia Shilingi Bilioni 4.1 huku akisema hadi Sasa wametoa jumla ya leseni za uvuvi 5336.

Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu imeanzishwa rasmi Mwaka 2010 lengo lake likiwa ni kusimamia shughuli zote za uvuvi wa Bahari Kuu na ufuatiliaji.


No comments: