OSHA WAONGEZA IDADI YA MAENEO YA KAZI KWA ASILIMIA 276 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 4 March 2023

OSHA WAONGEZA IDADI YA MAENEO YA KAZI KWA ASILIMIA 276

Mkurugenzi Mkuu wa OSHA Hadija Mwenda akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Jijini Dodoma 


 


Na Shakila Nyerere,Dodoma

maipacarusha20@gmail.com

Wakala wa usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) Wamefanikiwa Kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiriwa kutoka idadi ya 4,336 Hadi kufukia idadi ya 11,953 Nchin na kufanya ongezo kuwa kubwa kufikia asilimia 276


Akizungumza Jijin Dodoma mach 4/2023 na Wandishi wa Habari Mtendaji Mkuu wa wakala hiyo Hadija Mwenda amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt SAMIA SULUH HASSAN wakala wa usalama na afya mahali pa kazi(OSHA) umefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka idadi ya 4,336 hadi kufikia idadi ya 11,953 hapa nchini na kufanya ongezeko hilo kuwa kubwa na kufanya ongezeko la asilimia 276.


Hata hivyo amesema idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia kaguzi 322,241 sawa na asilimia 132 halikadhalika kumekuwa na ongezeko la asilimia 175 ya wafanyakazi waliopata mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kutoka wafanyakazi 32,670 hadi kufikia wafanyakazi 43,318.

“Mafunzo haya yanajumuisha mafunzo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na uundwaji wa kamati za usalama na mafunzo ya kufanya kazi za mazingira ya juu” Amesema Mwenda.


Mwenda amesema kumekuwa na ongezeko la upimaji afya za wafanyakazi kwa asilimia 320,upimaji afya kutoka wafanyakazi 363,820 hadi kufikia wafanyakazi 1,112,237 waliopimwa katika kipindi tajwa.

“Ongezeko hilo linatokana na kupunguza ada mbalimbali na kubadili mifumo ya usimamizi ambayo imewezesha meneo mengi ya kazi kukaguliwa na wafanyakazi wengi kupimwa afya na mafunzo mbalimbali kufanyika,ongezeko hili ni tafsiri kwamba hali ya usalama na afya katika maeneo ya kazi inazidi kuimarika”Amesema Mwenda.

Mtendaji Mkuu OSHA Amesema katika kusimamia sheria za usalama na Afya kwa lengo la kuzuia ajali,magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi maeneo ya kazi ambayo hayakuzingatia sheria na kanuni za usalama na afya yalichukuliwa hatua mbalimbali za kusheria zikiwemo kupewa hati ya maboresho ambapo maeneo ya kazi 1,588 yalipewa hati hizo na maeneo ya kazi mengine 105 yalitozwa faini.


Mwenda amesema kuwa Miongoni mwa majukumu ya OSHA ni kuchunguza ajali mbalimbali zinazotokea katika sehemu za kazi kwa lengo la kubaini vyanzo vya ajali ili kushauri namna bora ya kuzuia ajali kutotokea tena.


Aidha Mtendaji Mkuu OSHA Bi Mwenda amesema kuwa Katika kipindi cha miaka miwili ajali zilizoripotiwa zimepungua kwa asilimia 13.2 kutoka ajali 2,138,magonjwa yatokanayo na kazi yalipungua kwa asilimia 22.1 kutoka magonjwa 140 kufikia Mgonjwa 109.


No comments: