SIKU HII YA WANAWAKE DUNIANI ILENGE USAWA WA KIJINSIA NI KUTOKOMEZA UKATILI MJINI KIBAHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 8 March 2023

SIKU HII YA WANAWAKE DUNIANI ILENGE USAWA WA KIJINSIA NI KUTOKOMEZA UKATILI MJINI KIBAHA

 

Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha.





 

 

JULIETH MKIRERI ,MAIPAC KIBAHA


maipacarusha20@gmail.com 


IMEELEZWA kuwa lengo la usawa wa Kijinsia ni kutokomeza Ukatili na Ubaguzi dhidi ya Wanawake na wasichana na kuhakikisha wanapata fursa sawa katika umiliki wa rasilimali .


Hayo yameelezwa mjini Kibaha na Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Nickson wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha.


Amesema pamoja na mambo mengine ili kufanikisha lengo hilo ifikapo 2030 Serikali ina wajibu wa kuondoa aina zote za ukatili na ubaguzi dhidi ya Wanawake na Wasichana kwa kutekeleza na kutambua matendo hatarishi na kutoa huduma stahiki kwa walioathirika.


Katika hotuba iliyosomwa na Katibu Tawala huyo imeeleza kuwa Serikali ina wajibu wa kujumuisha masuala ya kijinsia katika shughuli za Serikali za Mitaa ili kukabiliana na vikwazo vinavyowakabili wanawake.


Aidha amesema katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani iendane na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango wa Wanawake katika kuleta maendeleo.


Amesisitiza kuwa Usawa wa Kijinsia na uwezeshaji wanawake na wanaume ni nyenzo muhimu kwa mqendeleo ya taifa lolote duniani .


Ofisa maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Kibaha Leah Lwanji amesema kuwa kipindi cha mwaka 2021/2022 wajasiriamali kwa makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu walikopeshwa mikopo yenye thamani ya sh. Mil. 894.8 kwa vikundi 158. 


Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa fedha hizo siyo kwa ajili ya kugawana bali ni za kuzalisha ili watu wengine nao waweze kukopa.

No comments: