Mkuu wa wilaya ya Monduli Joshua NASARI akipokea mizinga ya nyuki iliyotolewa na HIFADHI YA Taifa Ziwa MANYARA kwa wakazi wa Kijiji Cha Esilale |
Mkuu wa wilaya ya Monduli Joshua NASARI akizungumza katika uzinduzi WA mradi |
Na Pamela Mollel,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Hifadhi za Taifa Tanapa kupitia hifadhi ya ziwa Manyara imewapatia vikundi vitano mizinga ya nyuki 200 yenye thamani ya shilingi Milioni 23 lengo ikiwa ni kuongeza kipato pamoja na kutunza mazingira
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Esilalei kilichopo Wilayani Monduli Mkoani Arusha,Mkuu wa Wilaya hiyo Joshua Nassari alipongeza hifadhi hiyo kwa kuja na mradi wa kuwawezesha wananchi kiuchumi
Alisema kuwa zao la asali ni biashara kubwa sanaa ndani ya nchi lakini pia nje ya nchi hivyo ni vyema wakasimamia vizur mradi huo pamoja na kuzingatia suala la vifungashio bora litakalo saidia soko lao kukuwa kwa haraka
"Tunatamani siku moja tuwe na kiwanda kikubwa cha kuchakata asali hapa kijiji ambacho kitaweza kutoa kutoa ajira hata kwa watoto wenu"alisema Nassari
Aidha aliongeza kuwa soko la asali lipo kutokana na eneo hilo kuzungukwa na hoteli za kitalii lakini pia uwepo wa watalii ambao huja nchini kufanya utalii wa asili
Pia aliwataka wananchi hao kushirikiana na hifadhi hiyo pamoja na kuwaomba kutoa taarifa wanapoona viashiria vyovyote vya ujangili
Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu katika hifadhi ya ziwa Manyara,Kamishna Msaidizi wa uhifadhi Neema Mollel alisema idara ya mahusiano katika hifadhi hiyo inatumika kushirikiana kwa karibu na jamii pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi katika vijiji vyote vinavyozunguka hifadhi ya ziwa Manyara
Alisema kuwa mradi huo umeletwa mahususi katika kijiji hicho kutokana na uoto mzuri wa miti ambao utawawezesha nyuki kufika eneo hilo kwa urahisi na kuzalisha asali
Aidha alitaja lengo la mradi huo kuwa ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwenye maeneo yao na wananchi wawe mstari wa mbele kwa kuhakikisha hawachomi miti ovyo,hawakati miti ili kuhakikisha maeneo hayo yanaendelea kuwa na uoto wa asili jambo litakalosaidia vyanzo vya maji kuendelea kuwepo
Alitaja lengo lingine la mradi huo ni kuongeza kipato kutokana na zao la nyuki ambalo ni asali kwa kuongeza kipato moja kwa moja kwa wananchi lakini pia kutoa tiba za kitamaduni
"Asali inatumika sanaaa katika jamii ya kimaasai kutengeneza dawa za kifua,dawa za kina mama pamoja na kuweka ulinzi ikiwemo kufukuza wanyama wakali wasifike katika makazi ya wananchi, "alisema Mollel
No comments:
Post a Comment