TARURA KUMALIZA KERO YA BARABARA ZEGERENI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 11 April 2023

TARURA KUMALIZA KERO YA BARABARA ZEGERENI

 

Mmoja WA waendesha pikipiki akizungumza kero ya barabara hiyo

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji akizungumza na Waandishi wa Habari 

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji akizungumza na Waandishi wa Habari 

NA JULIETH  MKIRERI, MAIPAC KIBAHA



KERO ya barabara katika eneo la Zegereni ambako kuna uwekezaji wa viwanda mbalimbali inakwenda kumalizika Julai mwaka huu utakapokamilika mradi wa ujenzi wa Km 12.5 kwa kiwango cha lami.

Kwa muda mrefu eneo hilo limekuwa likilalmikiwa kuwa kikwazo kwa baadhi ya wawekezaji kukwama kufikisha malighafi zao viwandani kwa wakati hususani kipindi cha mvua.

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji amesema barabara hiyo ikikamilika itawezesha wawekezaji kusafirisha malighafi na bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo kwa wakati.

Mhandisi Runji ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo ya Visiga- Zegereni -Misugusugu inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Amesema barabara hiyo ilianza kujengwa Machi 2022 na Mkandarasi China Railway Seventh Group inatarajiwa kukamilika Julai 20 kwa gharama ya sh. Biln 16.8.

Mhandisi Runji amesema ujenzi wa barabara hiyo hadi sasa umefikia asilimia 75  na kwamba tayari  Mkandarasi amelipwa sh.biln nane.

Amesema katika eneo hilo la uwekezaji kwasasa vipo viwanda vikubwa 31 katika eneo lenye ukubwa wa ekari 1200 ambalo limepimwa kati ya ekari 5,297 zilizopo Zegereni.

"Serikali iliahidi kutatua vikwazo kwa wawekezaji na hili linaendelea kufanyika katika kongani hii ya Zegereni sasa tatizo ka barabara linaenda kumalizika na kuwawezesha wawekezaji kusafirisha bidhaa zao bila kikwazo" amesema.

Mhandisi Runji amebainisha kuwa ujenzi wa barabara kiwango cha lami kwenye maeneo ya uwekezaji inafanyika pia katika eneo la Kwala ilipo kongani ya viwanda ambapo biln tano zitatumika kujenga Km.tano.

 Clemence Joseph mkazi wa Zogowale inapopita barabara ya lami Visiga- Zegereni hadi Misugusugu ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo kiwango cha lami ambayo awali ilikuwa ya vumbi na changamoto kubwa ilikuwa kipindi cha mvua.

Amesema kabla ya ujenzi wa barabara hiyo usafiri wa bodaboda walikuwa wakilipa sh. 3,000 hadi 4,000 kutoka zogowale hadi Visiga tofauti na sasa ambapo wanalipa sh. 1,500 na pia wenye nyumba za kupanga wameongezeka baada ya kuwa na barabara ya uhakika.

Naye Radhia Ismail amesema ujenzi wa barabara hiyo umeanza kuleta mabadiliko kiuchumi kwa wafanyabiashara zao kwani gharama za usafirishji zimepungua lakini pia watu wanaofika katika maeneo hayo wamezidi kuongezeka

No comments: