KILIMO IKOLOJIA KUWANUFAISHA WAKULIMA KATIKA MASOKO KIMATAIFA-, KULINDA AFYA ZAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 2 May 2023

KILIMO IKOLOJIA KUWANUFAISHA WAKULIMA KATIKA MASOKO KIMATAIFA-, KULINDA AFYA ZAO

Dr Angella mkindi akizungumza na katika mkutano wa wadau sekta kilimo ikolojia





Mwandishi wetu, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Wakulima nchini, wameshauriwa kujiunga na Kilimo Ikolojia, ambacho hakihitaji matumizi ya Pembejeo za kisasa  zenye viuatilifu vya sumu ya kuua wadudu ili kuweza kunufaika na soko kubwa la kimataifa la  mazao yanayotokana na kilimo hicho.


Kilimo hicho pia ni  rafiki kwa afya ya ardhi , afya ya mkulima lakini kinasaidia kutunza mazingira na bioanuwai ambao ni rafiki katika kilimo na uhifadhi wa mazingira .


Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo Ikolojia,wakiwepo wakulima, maafisa ugani na taasisi zinazojihusha na kutoa elimu ya kilimo hicho jijini Arusha jana, Dk Angella Mkindi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Technolojia cha Nelson Mandela,amesema  kilimo Ikolojia kina manufaa makubwa kwa afya ya binaadamu.


Dk Mkindi amesema hivi sasa kuna changamoto ya makubwa ya matumizi ya pembejeo za kilimo ambazo zina kiasi kikubwa cha sumu, jambo ambalo linaathiri afya za walaji, wakulima na hata ardhi.


Mratibu wa miradi ya kilimo Ikolojia wa taasisi ya tafiti  Biovision  Africa Trust,Fredrick Ochieng  amesema ni muhimu wakulima kujiunga na kilimo hicho, kwani soko la mazao yake ni kubwa na ni rafiki wa afya za binaadamu.


Ochieng amesema wakulima wanaweza kupata elimu ya kilimo hicho, kupitia taasisi zilizopo nchini, ikiwepo kupitia jarida la Mkulima Mbunifu ambalo limekuwa likisambazwa bure kwa wakulima na taasisi mbali mbali.


Mratibu wa miradi wa taasisi ya Farm Radio, Susuma Susuma  alisema kilimo ikolojia pia ni muhimu kwa sasa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.



Susuma amesema kilimo ikolojia kinahimiza matumizi ya mbegu za asili,mbolea na asili na dawa za kuuwa wadudu za asili ikiwepo majani ya mti wa  mwarobanini  na kilimo hicho hakihitaji kununua mbegu kila msimu.


Mkulima  Charles Sautian  wa Kijiji cha Lengijave wilaya ya Arumeru, alisema tangu amejiunga na kilimo ikolojia ameongeza uzalishaji wa mazao lakini anapata soko kubwa la mazao yake.


Sautian anasema kwa sasa analima heka moja  ya mahindi kwa kilimo hicho na kupata gunia  28 na anapata masoko ya uhakika lakini pia familia yake inakula chakula ambacho ni salama.


Kilimo ikilojia tayari kimeanza kuwanufaisha mamia ya wakulima nchini ambao wamekuwa na uhakika wa soko la mazao yao.





No comments: