SERIKALI AFRIKA MASHARIKI ZATAKIWA KUONDOA VIKWAZO VYA AJIRA KWA WAFANYAKAZI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 9 May 2023

SERIKALI AFRIKA MASHARIKI ZATAKIWA KUONDOA VIKWAZO VYA AJIRA KWA WAFANYAKAZI

 

Mkutano Mkuu wa Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha

Msajili wa vyama vya wafanyakazi Nchini TANZANIA Bi. Pendo Zacharia Berege akizungumza KATIKA Mkutano WA mwaka WA Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki 

MAKAMU mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki Dokta Francis Atwol akizungumza KATIKA Mkutano Mkuu wa Mwaka WA Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki Jijini Arusha mapema leo

Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi nchini Tanzania (Tucta) Ndugu Henry Mkonda akiwakaribisha viongozi wa mashirikisho ya wafanyakazi WA Nchi za Afrika Mashariki katika mkutano Mkuu wa Mwaka WA Shirikisho la Wafanyakazi Afrika Mashariki Jijini Arusha mapema leo.


Na: Andrea Ngobole, Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Shirikisho la wafanyakazi Afrika mashariki limeziomba SERIKALI zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki kuondoa vikwazo vya vibali vya kufanya kazi kwa wanaafrika Mashariki katika Nchi zote zinazounda jumuiya hiyo.


Wakizungumza Leo katika mkutano Mkuu wa Mwaka unaofanyika Jijini Arusha na kuwezesha na shirika la kazi Duniani (ILO) wamesema vikwazo vya kisheria vya kufanya kazi katika nchi Wanachama vinarudisha nyuma juhudi za kuwakwamua wafanyakazi na Hali duni za Maisha.


MAKAMU mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki Dokta Francis Atwol ambaye pia ni mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi Kenya amesema umoja wa vyama vya wafanyakazi Afrika Mashariki ni muhimu sana kuimarika katika Nchi zao ili kuwa na Shirikisho imara linalotetea wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki.

Amesema itapendeza mtanzania mwenye sifa za kufanya kazi nchini Kenya kusiwe na vikwazo vya vibali vya kufanya kazi katika Nchi ya Kenya au mkenya akipata kazi Uganda kusiwe na vikwazo vya vibali kwani wote ni wanaafrika Mashariki.


Shirikisho Hilo linaundwa na vyama vya wafanyakazi  Toka Nchi zote zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki.

Msajili WA vyama vya wafanyakazi Nchini Tanzania, Pendo Zacharia Berege amesema Kuna uhuru na utulivu mkubwa kwa vyama vya wafanyakazi Nchini TANZANIA kwani vinazingatia kanuni na taratibu za kutetea haki za wafanyakazi.

Amewapongeza Shirikisho la Wafanyakazi Afrika Mashariki kwa kuheshimu katiba Yao na kuwataka kuwa na mshikamano na mashirikisho ya Nchi zote ili kujua changamoto mbalimbali za wafanyakazi katika Nchi Moja na nyingine ili kuzitafutia suluhisho la pamoja.


Amevitaka vyama vya wafanyakazi Nchini kuepuka migogoro baada ya uchaguzi ili kutekeleza vema jukumu la kutetea wafanyakazi na siyo kuwa kama vyama vya siasa kwani mwisho WA siku wafanyakazi huona vyama havipo kwa ajili ya kuwasaidia na kuwatetea na hivyo kushindwa kupata Wanachama wapya.


Amesema vyama hivyo vinapojenga mahusiano mema na wafanyakazi na SERIKALI vitatengeneza taswira nzuri itakayowavutia Wanachama wengi na kuwa na Sauti Pana zaidi  kwa maslahi mapana ya wafanyakazi.


Awali akiwakaribisha viongozi WA mashirikisho ya wafanyakazi Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi nchini Tanzania (Tucta), Henry Mkonda Amesema kuwa mkutano huu wa Mwaka ni vema ukaja na mkakati imara utakaoangazia changamoto za wafanyakazi katika Nchi zote ili kuwa na Sauti Moja itakayowasemea wanaafrika Mashariki.


Amesema mfano TANZANIA bara hawajui changamoto za wafanyakazi WA Zanzibar  Hali kadhalika Shirikisho la wafanyakazi Zanzibar hawajui changamoto za wafanyakazi WA bara kama ambavyo wa Kenya hawajui changamoto za Uganda.



Viongozi Hawa WA Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki wanakutana Arusha kwa muda wa siku mbili kuweka mkakati imara WA kusaidia changamoto za wafanyakazi Afrika Mashariki wakishrikiana na shirika la kazi Duniani (ILO)



No comments: