Profesa Assad ashauri wakurugenzi wa Bodi Mashirika ya Umma kupatikana kwa kuomba kazi na kufanyiwa usaili. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 21 August 2023

Profesa Assad ashauri wakurugenzi wa Bodi Mashirika ya Umma kupatikana kwa kuomba kazi na kufanyiwa usaili.

 

Profesa Mussa Assad



Na: Mwandishi wetu, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali ,Profesa Mussa Assad  ameshauri Wajumbe wa bodi za Mashirika ya Umma nchini, wapatikane kwa kuomba kazi hiyo na kufanyiwa usajili kuboresha Utendaji kazi wao.


Akitoa mada juu ya Uendeshaji wa Mashirika ya Umma na tafakuri kuhusu Tanzania, katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha(AICC) katika mkutano wa watendaji wa Mashirika na Taasisi za  Umma nchini,amesema upatikanaji wa wajumbe wa bodi ni tatizo


Profesa Assad amesema ili bodi za Mashirika ya Umma kufanya kazi kwa ufanisi ni lazima wajumbe wanaopatikana wawe uwezo wa kusaidia Taasisi.


Amesema pia matatizo mengine yaliyopo kwenye mashirika ya Umma ambayo yamesababisha kufa kwa mashirika ama kufanya kazi chini ni kiwango ni matumizi mabaya ya fedha na Rasilimali za Taasisi.


Profesa Assad amesema pia kuna  Matumizi mabaya ya fedha za Mashirika ikiwepo ununuzi wa magari ya kifahari ikiwepo V8 ya mwaka 2023 na Kila Mtendaji wa Serikali kuwa na magari hayo.


"Kuna haja gani kuwanunuliwa watendaji watano katika Taasisi Moja magari matano ya kisasa V8 ambapo inabidi kuajiri madereva, lazima maeneo ya kuegesha magari"amesema


Amesema sio Kila wakati maafisa hao wote watakuwa safarini wakitumia magari hivyo inapaswa kuwa na magari machache hata matatu na watendaji wakatumia kwa zamu.


"Lakini pia kuna hili nimeona tunakuja Arusha kwenye mkutano watendaji na wanakuja na ndege na magari yanawafata Arusha ili waje kutembelea nadhani hii pia ni matumizi mabaya ya Rasilimali za Mashirika "amesema


Amesema pia kuna tatizo la bodi na watendaji wa mashirika kuingiliwa na viongozi juu wa Serikali na hivyo kutolewa maamuzi ambayo yanaathiri mashirika.


"Kwa mfano tunanunua ndege Dreamliner ambazo tunajua kabisa matumizi yake hatuwezi kwani ndege ambazo zinahitajika sana ni za kufanya safari za ndani matokeo yake Shirika kupata hasara"amesema

Zitto Kabwe


Akitoa mada kuhusiana na mashirika ya Umma, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe alipendekeza watendaji wa mashirika ya Umma kuajiriwa na bodi.


"Mapendekezo yangu Mimi ni kuwa Rais akiteua Mwenyekiti wa Bodi ,basi bodi ndio ipewe jukumu la kuajiri Mtendaji Mkuu wa Shirika ili aweze kuwajibika kwa bodi"amesema.


Zitto amesema kumekuwepo na mgongano baina ya bodi na watendaji hao kwani kila mmoja ameteuliwa na Rais.


"Bodi ikiajiri Mtendaji Mkuu inauwezo wa kumuondoa kama atashindwa kutekeleza majukumu yake na kuajiri Mtendaji mwingine"amesema.

No comments: