Akili Bandia yatishia ajira za mamilioni - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 30 September 2023

Akili Bandia yatishia ajira za mamilioni

  



Musa Juma Mkurugenzi wa Maipac akitoa maoni katika kongamano la kikanda la Ulinzi na Usalama kwa wanahabari lililoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) jijini Arusha,


Kishimui Laizer , Arusha 


maipacarusha20@gmail.com


Technolojia mpya ya akili Bandia(AI) ambayo matumizi yake yameanza kuongezeka Maeneo mengi Duniani ikiwepo Tanzania.sasa imeanza kitishia ajira za mamilioni ya watu .


Technolojia hii ambayo inapatikana kupitia mitandao  inatumika hivi sasa, kuandika habari na jumbe mbalimbali,kunakili picha za watu,,kutangaza habari,kutoa takwimu, kujibu maswali mbalimbali ,kuandika barua na kujibu  kwa lugha mbalimbali.


Akili Bandia pia kwa sasa inatumika kurekodi mienendo ya kesi Mahakamani, kutoa huduma za ushauri na kuandaa matangazo ya aina mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mtu.


Wakizungumza katika kongamano la kikanda la Ulinzi na Usalama kwa wanahabari lililoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) jijini Arusha, Mtendaji Mkuu wa Taasisi Nucta Africa Nuzulack. Dausen , Mkurugenzi wa mafunzo wa baraza la Habari la nchini Kenya (MCK) ,Victor Bwirena na Mjumbe wa Bodi ya baraza la Habari nchini(,MCT) Jaji  mstaafu Robert Makaramba   walisema ni kuijua Technolojia ya akili ni kwani ni jambo la kidunia  kwa sasa.


Dausen alisema kwa sasa suala la Matumizi ya Akili Bandia ni la kidunia hivyo haliwezi kukwepeka na muhimu ni kujiandaa vyema kukabiliana nalo kwani lina faida na hasara zake.


Amesema ni ukweli kuwa matumizi ya Akili Bandia yanakwenda kuathiri ajira sio kwa wanahabari tu bali katika sekta mbalimbali lakini pia kutakuwa na ajira mpya za wataalam wa.Akili Bandia.


"Katika Vyombo vya habari itapaswa Sasa kuwepo na watalaam wa kufatilia masuala ya Akili Bandia lakini pia Sasa kuna haja ya kuboresha Sheria za habari lakini pia elimu ambayo inatolewa vyuoni kuingiza suala hili"amesema


Jaji Makaramba amesema, suala la Akili Bandia na matumizi ya Roboti Sasa vimeanza kutumika Mahakama za nje katika Mahakama ambapo tayari Kuna nchi wanatumia kusikiliza kesi na kutoa maamuzi"amesema


Alisema kwa sasa ni muhimu kuwepo maboresho ya sheria mbalimbali ili kuweza kuitumia Technolojia hii kwa faida badala ya kuleta changamoto kubwa.


Mkurugenzi wa mafunzo wa baraza la Habari la nchini Kenya (MCK) ,Victor Bwire  alisema tayari Kenya wemeunda kikosi kazi Cha kuanza kushughulikia suala la Matumizi ya Akili Bandia.


Bwire alisema, kuna haja kuanza Sasa mikakati ya maboresho ya sheria mbalimbali ili kwendana technolojia za kisasa badala ya kuwa na sheria ya kukandamiza Uhuru wa habari.


Katibu Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania (MCT),Kajubi Mukajanga aliwataka wanahabari kuanza kujiandaa sasa na matumizi ya Technolojia mpya.


Hata hivyo,Mukajanga alisema MCT imeridhishwa sana kongamano hilo kwani wanahabari katika ukanda wa Afrika Mashariki wameshiriki wamejumuika na kubadilishana uzoefu.


Mkurugenzi wa Taasisi ya usaidizi ya jamii za pembezoni (MAIPAC) Mussa Juma akichangia mjadala huo alisema suala la Akili Bandia linapaswa kujadiliwa kitaifa katika sekta mbalimbali.


"Juzi nilikuwa katika Maadhimisho ya siku ya Utalii Duniani suala la Akili Bandia pia lilizungumzwa ambapo mawakala wa Utalii walitakiwa kuanza kujifunza kutumia Technolojia hiyo"alisema


Hata hivyo alisema ni muhimu Sasa kuanza kufanyika maboresho ya sheria za habari na hata  maadili kwa wanahabari na wanataaluma wengine wanapotumia AI.


Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini(JOWUTA) pia alizungumzia maslahi duni ya wanahabari  kuwa ni suala la kiusalama kwa wanahabari.


Awali, Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari wanawake nchini(TAMWA) Dk Rose Reuben na Katibu Mtendaji wa muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini(UTPC) Kenneth Simbaya walieleza umuhimu wa kuzingatiwa suala la ulinzi na Usalama kwa wanahabari.


Kwa pamoja walieleza Taasisi hizo kufanyakazi kadhaa kuimarisha suala la Ulinzi na Usalama kwa wanahabari nchini Tanzania.




No comments: