DC KIBAHA AWATAKA WANANCHI KUFANYA USAFI KATIKA MAKAZI NA MAZINGIRA YAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 16 September 2023

DC KIBAHA AWATAKA WANANCHI KUFANYA USAFI KATIKA MAKAZI NA MAZINGIRA YAO




NA: BYARUGABA INNOCENT, MAIPAC KIBAHA.


maipacarusha20@gmail.com 


 MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amewaongoza mamia ya Wananchi kuadhimisha siku ya usafishaji kwa  kufanya usafi kwenye Soko la Loliondo.


Pamoja na Mambo mengine Simon ametoa rai kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya usafi kwenye Makazi yao pamoja na sehemu za  biashara ili kuimarisha ustawi wa afya zao kwani uchafu na chakula hayaendani.


"Wasiofanya usafi usafi wataondolewa,ni jambo la kusikitisha Sana,tena la aibu kwa sehemu ya Chakula kuwa chafu.Mama lishe asiyeweza kwenda na kasi ya usafi,atupishe"amesema Simon


Aidha, Simon ametoa wito kwa Mkurugenzi kuhakikisha Sheria ndogondogo zinaimarishwa hasa faini za ukusanyaji taka,uzoaji,ulipiaji na upelekaji dampo ili kuendana na wakati wa Sasa na kuimarisha kwa misingi ya usafishaji Mazingira


Asumpta Maziku ambaye ni mfanyabiashara wa nguo kwenye Soko hilo amewakumbusha wenzake kujiwekea utaratibu rafiki wa kusafisha Mazingira kwani uwepo wa Mazingira machafu huwakimbiza hata wateja kwa kuhofia kuhatarisha afya zao



Mwenyekiti wa Mama lishe Sauda Hassan amesema kuanzia Sasa Mama lishe wataanza kutekeleza usafi kwa vitendo ambapo kila Mama lishe atapaswa kuwa na vyombo maalum vya kuhifadhia taka huku Mkuu wa Wilaya akiwataka wote ambao hawataweza kwenye falsafa ya usafi kuwapisha wengine wanaoweza kuendelea kujitafutia riziki eneo Hilo ambalo limeajiri akina Mama wengi.


Diwani wa Kata ya Tangini Mfalme Kabuga ametoa rai kwa wafanyabiashara na wananchi wa Kata ya Tangini kufuata Sheria na kwamba yeyote atakaidi hatua za Kisheria zitachukuliwa.


Kila Septemba 16 ya kila Mwaka Dunia nzima hushiriki kwenye zoezi la usafishaji ikiwa ni ishara ya kukabiliana na Uchafuzi wa uharibifu wa Mazingira.



No comments: