EAC YAJIPANGA KUDHIBITI VIKWAZO VYA KIBIASHARA KWA NCHI WANACHAMA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 13 September 2023

EAC YAJIPANGA KUDHIBITI VIKWAZO VYA KIBIASHARA KWA NCHI WANACHAMA





Na Mwandishi Wetu, Arusha

maipacarusha20@gmail.com


JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC),imelenga kutekeleza mikakati kadhaa itakayosaidia kuongeza ufanisi katika Sekta za kibiashara hususani kwa kuendelea kupunguza vikwazo vilivyopo sasa.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Katibu Mkuu wa EAC,Dk.Peter Mathuki wakati akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa mipango, changamoto ya jumuiya hiyo alisema katika kuwezesha usafirishaji huru wa bidhaa kwa nchi wanachama vikwazo 26 vimeondolewa kutoka 33 vilivyokuwepo awali na kubakia saba pekee ambavyo navyo vinafanyiwa kazi.



Alisema kwa miaka miwili iliyopita walikuwa na vikwazo takribani 184 na sasa vimebaki saba ambavyo vinaonyesha wazi wazi kuna nguvu kubwa inafanyika na yote ni kutokana na nchi zote kuchangia pakubwa katika kufanikisha ilo.



Aliongeza kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo imefanya biashara kwa EAC kuongezeka kwa asilimia 13.4 hadi dola za Marekani bilioni 74.1 mwaka 2022 kutoka dola za Marekani bilioni 65.3 mwaka 2021, wakati jumla ya biashara ya ndani ya EAC, biashara imeongezeka kwa asilimia 11.2 na kuwezesha kupata dola za Marekani bilioni 10.9 mwaka 2022 kutoka dola bilioni 9.8 mwaka 2021.



“Kufanya biashara kwa pamoja kwa ndugu zetu kumeongeza uchumi kwani mwaka 2022 tulifikia asilimia 15 na mwaka huu 2023 muelekeo umekuwa ni mzuri kwani tumepata asilimia 16 mwezi Januari na asilimia 19 mwezi Februari”,alisema Mathuki.



Aliongeza kuwa kwa sasa wanaangalia namna ya kutumia safaru ya pamoja ambayo itafanya uchumi wa Afrika Mashariki kukua lakini pia kuondoa changamoto mbali mbali ambazo wananchi huwa wanakumbana nayo kwenye mipaka ya nchi hiyo ikiwemo ile ya kubadilisha fedha kwanza lakini pia wanapanga namna gani nchi zote zitatumia kitambulisho cha pamoja.



Alitumia fursa hiyo pia kuweka wazi kuwa Baraza la Mawaziri la EAC imepanga kuwa na mazungumzo kuanzia Agosti 22 hadi Septemba 2023 kuweza kujadili kuhusu nchi ya Somalia kupewa uanachama rasmi.



Kuhusu mchakato wa kurejesha amani Mashariki mwa DRC Congo, alisema wanaendelea na safari hiyo kwa kujitolea ikiwemo majeshi ya EAC ambapo pia ameipongeza Umoja wa Afrika (EU), na ile ya Ulaya (EU),kwa kutambua mchango wao kuleta amani na kuamua kutoa sapoti.





No comments: