Gwimile Azitaka kamati kulipa mafundi kwa wakati - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 10 September 2023

Gwimile Azitaka kamati kulipa mafundi kwa wakati

 

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Michael John Gwimile




Na: Mwandishi Wetu, Rufiji


maipacarusha20@gmail.com


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Michael John Gwimile amefanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ikiwemo shule zinazojengwa na Serikali na kuzitaka kamati za ujenzi kuwalipa Kwa wakati Mafundi wa miradi hiyo.


Ameyasema hayo Septemba 8, 2023 wakati akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika kata ya Utete,Mgomba, Chemchem na Umwe.


“kitu ambacho sisi hatutaki ni kwamba tusianze kutengeneza madeni mapya kama hela imekuja na ni kwa ajili ya mradi na hawa Watu wapo site wawe wanalipwa kwa wakati. Hakuna haja ya kuwakopa Alafu jengo linaisha tunaanza kufuatana Halmashauri” amesisitiza Gwimile 


“levo yetu ya Halmashauri nyie wakuu wa idara ni na usimamizi wa kamati na kugaidi kamati, Injinia, Mtu wa Elimu, Manunuzi ni kuishauri kamati ndo kazi yenu, tusiiiamulie tuishauri” ameongeza.


Wakizungumza baada ya ukaguzi huo Wananchi  wanaoishi maeneo hayo wamesema wameridhishwa na namna wanavyoshirikishwa katika kamati za Ujenzi .


“tumeridhishwa na ushirikishwaji wake, sisi tunaotoka kwenye jamii ya kawaida tupo kama wane tukishirikiana na viongozi wengine kutoka idara mbalimbali za kiserikali, kwahiyo tafsiri yake ni kwamba tuligawanywa kwenye kamati kuu mbili mimi mwenyewe nikiwa kwenye kamati ya mapokezi” amesema Ali Kisongo Kisongo Mkazi cha Mgomba Kaskazini.


Suna Idd Mtulia Mkazi wa Kata ya Mgomba ambae pia ni mjumbe wa kamati ya Ujenzi wa shule mpya ya msingi Mgomba ameishukuru Serikali kuwajengea shule hiyo ambayo kukamilika kwake kutaondoa adha ya watoto kusafiri umbali mrefu huku wakisindikizwa na wazazi wao na kuwasubiri watoke shuleni.


“yaani wengine wanatembea kilometa 3 kama wanaoishi katika Kijiji cha Mpima lakini wanaotoka Mapwegele wanatembea kilomita 6 kwenda Shule. Kwahiyo tunashukuru Mpima kuna Shule kwahiyo wanaotoka kule nafikiri sasa hivi watakuwa kulekule, hasa kwa hawa wadogowadogo wanaotaka kusoma chekechea, wanaotoka Mapwegele pia kuna Shule inajengwa kwahiyo changamoto itapungua kwa wazazi kuwaleta shule asubuhi” amesema mtulia.


Akielezea fursa zinazopanatikana kutokana na Ujenzi wa shule hizo Abdallah Makongora Mkazi wa Chemchem amesema uwepo wa miradi hiyo unachangia kutoa fursa za ajira na uwepo wa shughuli na kujipatia kipato.


“kama sasa hivi wageni wapo kibao, Dada zetu wamejenga migahawa hapa, vijana nao pia tunapata visenti na ajira, unakuja kufanya kazi hapa unapata chochote kitu” amesema Makongora.

No comments: