Jengo refu kuliko yote Arusha, Kizinduliwa kesho na Rais Samia - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 1 September 2023

Jengo refu kuliko yote Arusha, Kizinduliwa kesho na Rais Samia

  








Na: Andrea Ngobole, MAIPAC 


 maipacarusha20@gmail.com


Jengo refu kuliko yote kwa sasa katika Jiji la Arusha ambapo limejengwa na umoja wa posta barani Afrika (PAPU) litazinduliwa kesho na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

 Akizungumza na waandishi wa habari Leo September mosi, 2023, Mkuu wa mkoa Arusha, John Mongella amesema sherehe za uzinduzi wa jengo Hilo lilipo pembeni mwa mount Meru Hotel zitafanyika kuanzia asubuhi.


Mongella amewataka wakazi wa Arusha kujitokeza katika mapokezi ya Rais Samia Suluhu Hassan na kufatilia uzinduzi huo wa kihistoria


Mongella amesema uwepo wa jengo la PAPU katika Jiji la Arusha ni moja ya ongezeko la vivutio vya Utalii vilivyopo mkoani humo, hivyo ni vema kila mtu  akajivunia uwepo wa jengo hilo.


Amesema serikali  imejipambanua katika kuleta  mageuzi makubwa katika kusukuma uchumi wa nchi kwa kuboresha  sekta zote ikiwemo ya  posta.


"Uwepo wa jengo hili Arusha ni fahari kwa nchi yetu kwani inatuongezea  utalii mwingine,uzuri wake unavuta watu mbalimbali kuja kuliangalia, niwaombe wananchi tuje kuungana na kipenzi chetu Rais Samia kulizindua jengo hili,"amesema.

 

Naye Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo amesema posta wanavifaa vya kisasa yakiwemo magari,pikipiki na vingine ili kutoa huduma kwa urahisi na kisasa bila kumuingiza mteja hasara.


Mbado amesema uzinduzi huo unakwenda kuboresha huduma za posta barani Afrika naTanzania


No comments: