Polisi yacharuka na Kampuni binafsi za Ulinzi, wafanyakazi wote kuchukuliwa alama za vidole - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 16 September 2023

Polisi yacharuka na Kampuni binafsi za Ulinzi, wafanyakazi wote kuchukuliwa alama za vidole

 

  


Mlinzi anayetuhumiwa kwa wizina Kisha kutoroka na wezi

Mlinzi anayetuhumiwa kwa njama za wizi


Mwandishi wetu, Arusha

maipacarusha20@gmail.com



Jeshi la polisi mkoani Arusha, limecharuka kufuata walinzi wa Kampuni ya Mengwe kutajwa kuhusika na tukio la ujambazi na Sasa walinzi wote mkoa Arusha kuhakikiwa.


 Walinzi wawili wa Kampuni hiyo wanasakwa kuhusika na  ujambazi, kwenye makazi ya Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Predators Safari Club Ltd, Yusuph Khan eneo la Kiranyi Sakina mkoa Arusha.


Walinzi wa Kampuni hiyo pamoja na Watuhumiwa wengine wa wanatuhumiwa kuiba sh 30 milioni na vidani vya dhahabu vyenye thamani ya sh 15 milioni, septemba 10 na kukimbia .


 Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo amesema Jeshi hilo limeanza kuhakikisha wafanyakazi wa kampuni za ulinzi, kwa kuchukuwa alama za vidole na kupata taarifa zao ili kuzihifadhi.


"Tutapita kwenye hizi kampuni na kuchukuwa alama za vidole na taarifa za wafanyakazi kwani watu, wanakodisha  hizi kampuni za ulinzi ili walindwe lakini sio kuibiwa"alisema


Alisema kutokana na tukio hilo la wizi polisi bado wanaendelea na uchunguzi na tayari wakurugenzi wa kampuni ya Mengwe wamehojiwa na wametakiwa pia kushirikiana na vyombo vya dola kuwakamata watuhumiwa.


"Tumewahoji tayari na wameendelea kutupa ushirikiano, kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa"alisema


Meneja wa Kampuni wa Mengwe Security , Juma Masuka alisema wafanyakazi wawili wa kampuni hiyo,Moses Alfred Mabula(46) na  Lazaro Richard Pyuza(37) wanasakwa kwa tuhuma za kushiriki katika ujambazi.


"Bado tunawatafuta hawa walinzi ambao walionekana kwenye kamera za CCTV  wakiwa wanawafungulia geti majambazi lakini pia walishiriki kupora kwa kuwaweka chini ya ulinzi Khan na familia yake na baadae kukimbia"alisema


Alisema walinzi hao waliokuwa ni wakazi wa eneo la Daraja mbili wamekimbia tangu kufanya ujambazi huo lakini watahakikisha wanakamatwa na akatoa wito wananchi watakao waona kutoa taarifa polisi.


Kampuni ya Predators Safari imetangaza kutoa zawadi ya sh 2 milioni kwa ambao watafanikisha kukamatwa watuhumiwa hao.


No comments: