Na: Mwandishi Wetu, Lindi
maipacarusha20@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kwa uwekezaji iliyoufanya kwenye mji wa Kale wa Kilwa Kisiwani
Mhe. Rais amesema hayo akiwa wilayani Kilwa kwenye ziara ya kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.
Mhe. Rais aliongeza kuwa mji wa Kilwa Kisiwani ulikuwa mji wa kibiashara enzi za kale hivyo Serikali ina nia ya kuurudisha mji wa Kilwa kuwa mji wa Kibiashara Kama ulivyokuwa zamani kwa kuweka fedha nyingi katika kutengeneza miuondo mbinu Kama bandari ya uvuvi na utengenezaji wa vivutio vya Utalii vya Kilwa Kisiwani, Songomnara na Kilwa kivinje.
Vilevile Mheshimiwa Rais alisema kuwa uwekezaji kwenye bandari ya uvuvi ni fursa kwa wanakilwa kwani watakuwa na uwezo wa kujiingiza kwenye shughuli za utalii Kama wenyeji wa eneo hili.
"Nimeambiwa kuwa meli nne za watalii zimeshawahi kuja hapa Kilwa kwa ajili ya kuleta watalii kwa ajili ya kuja kutalii katika visiwa vya Kilwa Kisiwani na Songomnara" ameongeza Mhe. Rais.
Pia Mhe. Rais akitolea ufafanuzi juu ya suala la wanyama wakali na waharibifu amesema kwamba suala hilo amelichukua anaenda kulifanyia kazi akiwa na wataalamu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
No comments:
Post a Comment