RC Mongela Awaagiza Wakuu wa wilaya na wakurugenzi kukamilisha Miradi kabla ya December 31 mwaka huu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 6 September 2023

RC Mongela Awaagiza Wakuu wa wilaya na wakurugenzi kukamilisha Miradi kabla ya December 31 mwaka huu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza na watendaji wa wilaya zote za mkoa wa Arusha 


Watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela 


 Na Mwandishi Wetu, Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa Mkoa wa Arusha John  Mongela amewataka wakuu wa Wilaya zote Mkoani hapa, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara CMT kuhakikisha miradi ya Maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri zao inakamilika ndani ya wakati na Kwa viwango stahili.


Amesema hayo katika kikao Kazi cha wakuu wote wa Wilaya, Mabaraza ya Madiwani wa Halmashauri Pamoja na Wataalamu wa Idara za halmashauri zote, Makatibu Tawala Kamati za ulinzi na usalama za Wilaya zote ambapo amewataka kuhakikisha ifikapo Mwezi disemba 31 miradi yote iwe imekamilika.


Amesema kwamba uwepo wa miradi viporo Imekuwa suala mtambuka linalochelewesha kukamilika kwake hivyo Kutoa agizo la kuanzishwa kamati za usimamizi wa miradi kuanzia ngazi ya kata WDC Pamoja na wananchi utaosaidia kusimamia majukumu Kwa haraka na wakati.


"Naagiza kuanzia Sasa tukaanzishe kamati za usimamizi wa miradi ngazi ya kata WDCs Pamoja na Wilaya, Mkoa Kwa lengo la ugatuzi wa madaraka ya usimamizi Kwani inaonyesha huko Kuna wasimamizi Wazuri kutokana na uzoefu tuliopata na sio wale watendaji hata wananchi muwashirikishe kwenye hizi kamati" Alisema 


Amesema kuwa Mwaka wa fedha 2022 hadi 2023 Kuna miradi mingi viporo ambayo haijakamilika na mingine haijaanza hivyo kuwataka ifikapo disemba 31 mwaka huu miradi hiyo iwe imekamilika huku akiwataka kutojimilikisha kila jambo na kuunda Timu za usimamizi ngazi za kata .


Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala Amesema kwamba wapo tayari kuyafanyiakazi yale yote waliyoagizwa ikiwemo umaliziaji wa miradi na kuunda kamati za ufuatiliaji ngazi ya kata na Wilaya Kwa kuwashirikisha wananchi na WDC Ili kuleta matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo viporo.


Hata hivyo uundaji wa kamati ni mbinu mbadala katika utekelezaji wa miradi na kumiliki kwa pamoja viongozi na wananchi mnapokuwa na vikosi kazi hata vya watu wa kawaida kunakuwa na Ile umiliki wa pamoja hata kama viongozi tupo nikienda pale nitataka kujua kamati hiyo imekwama wapi.


Kwa Mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC Suleiman Msumi ameeleza kwamba Halmashauri yake Ina miradi yenye thamani ya takribani bilioni 3 na zaidi ambayo ipo kwenye sekta za Afya na Elimu ambayo inatekelezwa Kwa mapato ya ndani na wamejipanga kuhakikisha inatekelezwa katika muda uliopangwa.

No comments: