Taasisi za ardhi kutoka nchi 20 Afrika zinakutana jijini Arusha kujadili changamoto za umiliki wa ardhi. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 12 September 2023

Taasisi za ardhi kutoka nchi 20 Afrika zinakutana jijini Arusha kujadili changamoto za umiliki wa ardhi.



Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko afungua kongamano la Ardhi Afrika wito watolewa kusaidia Jamii za pembezoni kumiliki ardhi.




Mratibu wa TALA Bernard Baha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo



Mwandishi wetu, Maipac


maipacarusha20@gmail.com


Naibu Waziri Mkuu,Doto Biteko Leo amefungua kongamano la nne la Ardhi Afrika huku wito ukitolewa kusaidia Jamii za pembezoni kumiliki ardhi.


Kongamano hilo ambalo linafanyika Mountmeru hoteli jijini Arusha,linashirikisha watu zaidi ya 100 kutoka Mataifa 20 barani Afrika.


Akifungua Kongamano hilo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan,Naibu Waziri Mkuu Biteko alitaka sheria Bora za Ardhi barani Afrika ili kusaidia kutatua migogoro ya ardhi lakini pia kuwapa hati za umiliki ardhi wananchi.


Naibu Waziri Mkuu amesema ardhi ni moja ya mambo muhimu kwa sasa hivyo wananchi wasaidie kumiliki ardhi yao ili kuchochea Maendeleo.


Alisema serikali ya Tanzania imejipanga kutatua migogoro ya ardhi na kuhakikisha ardhi inapimwa na wananchi kupewa hati miliki.



Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi, Jerry Slaa alisema bara la Africa linaweza kutatua changamoto za ardhi na kuwezesha wananchi kutumia ardhi yao kupata Maendeleo.


Alisema kongamano hilo ni muhimu sana kwani linashirikisha Taasisi za Utawala na usimamizi wa ardhi Afrika kutoka Mataifa 20 barani Afrika.


Alisema lengo la kongamano hilo ni kuwa na Usalama wa umiliki wa Afrika.


Awali Rais wa Taasisi ya kimataifa  inayoshughukia Haki za umiliki wa Rasilimali (RRG) barani Afrika, , Dk Solange Badji alishauri Jamii za pembezoni kupata haki za umiliki wa ardhi.



 Badji alisema Jamii ya za pembezoni barani Afrika zinakabiliwa na changamoto ya umiliki wa ardhi ya Jamii.


Alisema Jamii hiyo licha ya kuishi katika ardhi kidogo lakini hawana hati miliki ya maeneo yao na hivyo kukosa Haki za umiliki kisheria.


Amesema Jamii hizo za pembezoni na nyingine za asili zimeathirika na mabadiliko ya Tabia nchi na kutaka kuwepo na sheria na Kanuni nzuri za umiliki wa ardhi.


"Napongeza serikali ya Tanzania kuwa na sheria na sera nzuri za ardhi ambazo zinasaidia kuondoa migogoro ya ardhi "alisema



Dk Badji amesema katika kusaidia Jamii za pembezo ni taasisi hiyo imetoa fedha kwa  mtandao wa Mashirika ya wafugaji wa asili na waokota matunda (Pingos Forums) na  Ujamaa Community Resource Team(UCRT) kuwezesha kwa mradi wa ardhi  kwa jamii za pembezoni.

Mwakilishi wa UCRT Makko akizungumza na waandishi wa habari 


Mwanzilishi wa shirika la UCRT,Makko Sinandei alisema ,wanatarajia kushirikiana na PINGOs Forums kusaidia upimaji wa ardhi za vijiji, utoaji elimu wa umiliki wa ardhi kwa jamii na utumiaji ardhi kiuchumi.


Mratibu wa mtandao wa Mashirika yanayojihusisha  na utetezi wa rasilimali ardhi(TALA) Bernard Baha alisema kongamano hilo lina umuhimu mkubwa kwani wanatarajia kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya umiliki wa ardhi barani Afrika.


Baha alisema katika kongamano hilo pia kila nchi inatarajiwa kutoa mikakati yake ya kukabiliana  suala la upatikanaji hatimiliki za ardhi na kukabiliana na migogoro ya ardhi .


Naibu Waziri wa Ardhi wa serikali za ya mapinduzi Zanzibar Juma Makungu alisema ardhi ni maisha na kuomba kongamano jingine kufanyika Zanzibar.



No comments: