Na Mwandishi wetu, Geita
WATU wenye ulemavu wamewataka wadau wa madini nchini kuwapa ajira kwenye sekta ya madini ili nao waweze kushiriki katika fursa hiyo kwani sheria imeelekeza hivyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Foundation for disabilities hope FDH, Michael Hosea ameyasema hayo katika siku ya ushirikishwaji watanzania kwa sekta ya madini kwenye maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini mjini Geita.
Hosea amesema watu wenye ulemavu hawapewi ushirikiano wa kutosha pindi fursa za ajira zikitokea kwani wanaoshindwa kupata kwani mawasiliano ni hafifu hawawafikii viziwi, wasioona inakuwa shida kupata mazingira jumuishi.
"Nawapongeza Stamico kwa kujali watu wenye ulemavu, sheria namba 9 ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 imeelekeza kila mwajiri atenge asilimia 3 za ajira kwa watu wenye ulemavu wao ninyi mmetekelezaje? amehoji Hosea.
Mwakilishi wa kampuni ya Busolwa Mining, Masumbuko Thomas amesema wameajiri watu watatu wenye ulemavu na wanawake 30.
Mwakilishi wa kampuni ya Geita Gold Mining Ltd, Reward Tenga amesema hana idadi ya wafanyakazi wenye ulemavu ila kati ya wafanyakazi wao zaidi ya 2,000 asilmia 2.3 ni wanawake.
Mkurugenzi wa shirika la madini nchini (Stamico) Dk Venance Mwasse amesema japokuwa watu wanafanya biashara na kutafuta fedha ila wasisahau ubinadamu.
"Tuwajengee uwezo watu wa makundi maalum kwani kuna kikundi cha watu wenye usikivu hafifu wamepatiwa elimu kule Mbogwe na wanachimba dhahabu hata kina mama wana fursa migodini wanaweza wapewe elimu na wakafanya kazi," amesema Dk Mwasse.
Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema amesikia maelezo na kilio cha makundi maalum na kwa vile sheria ipo atahakikisha anaisimamia.
"Ushiriki wao unapaswa uwe kwa asilimia 100 kwani wanatambulika kwa mujibu wa sheria hivyo makampuni yanapaswa kutenga nafasi zao," amesema Waziri Mavunde.
No comments:
Post a Comment