Biteko ataka wanasiasa kufanya siasa za kubadili maisha ya watu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 12 October 2023

Biteko ataka wanasiasa kufanya siasa za kubadili maisha ya watu




NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC CHALINZE


Maipacarusha20@gmail.com


NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amesema ili kuwa na maendeleo ni vema kufanya siasa za kubadili maisha ya watu badala ya siasa za maneno.


Vilevile amesema Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatakiwa kuacha kujiingiza kwenye matusi na kejeli badala yake wa waelezee yale yaliyofanyika kwenye maeneo.


Biteko ameyasema hayo jana mjini Lugoba alipokuwa akihutubia Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Wakazi wa Jimbo la Chalinze kwenye mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani uliondaliwa na Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete.


Naibu Waziri Mkuu huyo alisema muda huu ni wakuelezea Maendeleo yaliyofanyika na si kuishia kuongea na kuacha watu wengine kuzungujza maneno ya kejeli kwa Serikali iliyopo madarakani.


Kadhalika alisisitiza wanachama hao kuachana na siasa za utambulisho na kuwa na siasa za Maendeleo sambamba na kushirikiana kwa kila jambo kushikamana.


"Shikamaneni, thaminianeni na kuvumiliana angalieni yanayowaweka pamoja badala ya yale yanayowatenganisha tusiingie kwenye matusi na kejeli kazi yetu iwe ya kuyasemea yale yaliyofanywa na serikali" alisema.


Pia aliwataka Watumishi kushirikiana na wananchi kuwafuata walipo na kutagua kero zao badala ya kukaa kwenye madawati ofisini wakiwasubiri.


" Wananchi wanachohitaji ni huduma tuwapelekee maendeleo huko waliko rasilimali fedha zilizopo zitumike kwa kiwango kinachotakiwa"


Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mkuu huyo na Waziri wa Nishati ameagiza uongozi wa Tanesco Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye shule ya Sekondari Moreto ambapo aliahidi kupeleka kompyuta kumi ili wanafunzi hao waweze kusoma maomo ya sayansi.


Akizungumza katika mkutano huo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete ambae pia alikuwa mbunge wa kwanza jimbo la Chalinze alisema, uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu Biteko sio jambo la kushangaza kwani ni Naibu Waziri wa tatu sasa.


Alisema ,Rais Samia Suluhu Hassan amefanya chaguo sahihi kwa katumia Mamlaka yake ya kikatiba kuteua.


"Biteko fanyakazi zako,kwa mujibu wa katiba ya nchi,mwenye Mamlaka ya kufanya maamuzi ni Rais, na katumia Mamlaka yake ya kikatiba,midomo imeumbiwa kusema,waache waseme


Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema jimbo hilo katika utekelezaji wa ilani umefikia asilimia 96.



Kikwete alisema tayari sh. Biln sita zimepokelewa katika Halmashauri ya Chalinze kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo na kuondoa vikwazo vilivyokuwepo awali.


Akizungumzia upande wa Elimu Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliishukuru Serikali wakati anaingia katika nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo kulikuwa na shule za Sekondari 17 na sasa zinefikia 25 ikiwa ni ongezeko la shule nane.


Aidha alibainisha kwamba ujenzi wa shule za msingi umeongezeka na kuondoa kikwazo cha mlundikano wa wanafunzi darasani na sasa kufikia 113, huku zahanati zikiongezeka kutoka 36 hadi 61 na vituo vya afya ambavyo sita viko katika hatua ya ukamilishaji kutoka vinne vilivyokuwepo awali.


Kadhalika alisema huduma ya maji imeongezeka kutoka lita 7,500 hadi kufikia milion 21 vioski 114 hadi 1224 na wakazi wanaopata huduma sasa wamefikia asilimia 96 kutoka 62 za awali.


Kwa mujibu wa Kikwete upande wa nishati ya umeme shule za msingi 108 zimeunganishwa umeme Sam amba na Vijiji vyote 75 katika kata 15 za Halmashauri ya Chalinze huku akiwahamasisha wananchi kuwa na mwamko wa kuunganisha nishati hiyo.

No comments: