Na Mwandishi wetu, Geita
maipacarusha20@gmail.com
MWENYEKITI wa wanawake wanaofanya biashara ya kuuza na kununua magonga ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara (MIWOTAMA) Joyce Mkilanya ameshinda tuzo ya muongeza thamani bora wa madini.
Mkilanya amepatiwa tuzo hiyo kwenye usiku wa malkia wa madini katika maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini iliyofanyika mjini Geita.
Katibu wa chama cha wachimbaji madini wanawake Tanzania (TAWOMA) Salma Kundi amempongeza Joyce kwa kushinda tuzo hiyo ya muongeza thamani bora wa madini.
Kundi amesema Joyce anastahili pongezi kwa kushinda nafasi hiyo ya muongeza thamani bora wa madini na kupatiwa tuzo ya kutambua mchango wake kwenye sekta ya madini.
Akizungumza baada ya kupatiwa tuzo hiyo Joyce Mkilanya amesema anawashukuru wote ambao wameona anastahili kupata tuzo hiyo ya muongeza thamani bora wa madini.
"Nawashukuru viongozi wote walioona nastahili kupata tuzo hii pia nawashukuru wanawake wenzangu wa magonga kwa ushinikiano mkubwa wanaonipatia kwenye kazi zangu.
Amesema tuzo hiyo itakuwa chachu kwake katika kuongeza ari zaidi kwenye shughuli zake za biashara ya kuuza na kununua magonga ya madini ya Tanzanite.
Diwani wa Kata ya Mirerani, Salome Nelson Mnyawi amempongeza Mwenyekiti huyo Joyce kwa kupata tuzo hiyo ya muongeza thamani bora wa madini.
"Ametutoa kimasomo wanawake wa madini ya Tanzanite kwa kweli anastahiki pongezi nyingi na kudhihirisha kuwa ni mwanamke wa shoka na hata huo uenyekiti unamfaa sana," amesema Diwani Salome.
No comments:
Post a Comment