Na: Mwandishi wetu, Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Michuano ya 16 ya Chemchem CUP 2023 ambayo inalenga kupiga vita ujangili wa Twiga imezinduliwa Jana katika eneo la hifadhi ya jamii ya Burunge WMA wilayani Babati mkoani Manyara.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa wilaya ya Babati.Lazaro Twange kwa niaba ya Mkuu wa mkoa,alisema michuano hiyo licha ya kuinua vipaji vya michezo lakini inaendeleza uhifadhi.
Twange alisema vijiji 10 ambavyo vinaunda Burunge WMA, vinapaswa kushirikiana na Taasisi ya chem chem ambayo imewekeza shughuli za utalii na uhifadhi katika eneo hilo.
"Tunatarajia nyie muwe mabalozi wazuri wa uhifadhi ,mtowe taarifa za wanaojihusisha na ujangili lakini pia muendelee kunufaika na uhifadhi"alisema
Awali Mkurugenzi wa chemchem association Fabia Bausch alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa imekuwa na faida kubwa kushirikisha jamii katika uhifadhi kupitia uhifadhi.
Fabia alisema mwaka huu kwa mara ya kwanza kutakuwa na timu 10 za wasichana za mchezo wa soka, timu 16 za wanaume na timu 7 za vijana.
Amesema taasisi hiyo imetenga zaidi ya sh 99.2 million kufanikisha michuano ya mwaka huu.
Awali Mwenyekiti wa michuano hiyo, Elasto Belela amesema maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika ambapo timu zote shiriki tayari zimepewa seti za jezi na mipira kwa maandalizi.
Amesema mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya sh 2.5 milioni wa pili 1.5 milioni wa tatu 1 milioni na kwa upande wa wasichana mabingwa watapata 1.5 milioni, mshindi wa pili million Moja na mshindi wa tatu 500,000.
Kwa michezo ya vijana chini ya miaka 18 mshindi atapata milioni Moja wa pili 600,000 na WA tatu 400,000.
No comments:
Post a Comment