Timu 12 zatinga robo fainali chemchem CUP 2023. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 16 October 2023

Timu 12 zatinga robo fainali chemchem CUP 2023.

 




Mwandishi wetu.Babati.


Timu 12 za soka la Wanawake na wanaume zimetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya chemchem CUP 2023 baada ya kuongoza katika michezo katika Kanda tatu.


Timu hizo ni timu za  soka za wakubwa ,Timu za vijana na Timu za Wanawake wa soka ambapo kwa mara ya kwanza zimeshiriki michuano hii ambayo ilikuwa inashirikisha jumla ya timu 31.


Michuano wa chemchem ambayo mwaka huu inagharimu zaidi ya sh 100 milioni inadhaminiwa na Taasisi ya chemchem ambayo imewekeza shughuli za Utalii na uhifadhi katika eneo la hifadhi ya Jamii ya wanyamapori Burunge wilayani Babati.


Katibu wa chemchem CUP,John Bura amesema kwa Upande wa soka  wakubwa Timu ambazo zimeingia robo Fainali ni Macklion, Macedonia na Mdori FC.


Bura alisema timu nyingine ni Olasiti FC Manyara FC na Maweni FC.


"Robo fainali tunatarajia kuanza jumanne Octoba 17 ili kuelekea kwenye nusu fainali na baadae fainali"alisema


Alisema pia timu za vijana na wanawake ratiba itapangwa kwa ajili ya robo fainali ambapo miongoni mwa timu ambazo zimeingia ni pamoja nq Mwada Queen,Maweni Qeen majengo Mdori.


"Timu za vijana chini ya miaka 18 nazo zinashiriki ambazo ni pomoja na Mwada FC ,Ngolei FC,Magara FC,Mejengobnw Scopiaon ma Maweni"alisema


Awali  akizungumza siku ya uzinduzi wa michuano hiyo uliofanywa na Mkuu wa mkoa wa Manyara,Queen Sendiga, Mkurugenzi wa chemchem association Fabia Bausch alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa imejuwa na faida kubwa kushirikisha jamii katika uhifadhi.


Fabia alisema mwaka huu  kauli mbiu ni kupiga Vita ujangilimwa Twiga na kwa mara ya kwanza kutakuwa na timu 10 za wasichana na za mchezo wa soka, timu 16 za wanaume na timu 7 za vijana.


Amesema taasisi hiyo imetenga kutimia zaidi ya sh 100 million kufanikisha michuano ya mwaka huu.


Mwenyekiti wa michuano hiyo,Elasto Belela alisema  mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya sh 2.5 milioni. wa pili 1.5 milioni wa tatu 1 milioni .kwa upande wa wasichana mabingwa watapata 1.5 milioni,mahindi wa pili million Moja na mshindi wa tatu 500,000.


Kwa michezo kwa vijana chini ya miaka 18 mshindi atapata milioni Moja wa pili 600,000 na wa tatu 400,000 ambapo timu zote zimepewa seti ya jezi na mipira.

No comments: