WAZIRI MHAGAMA AZINDUA WIKI YA VIJANA YA KITAIFA MANYARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 11 October 2023

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA WIKI YA VIJANA YA KITAIFA MANYARA

 



Na Mwandishi wetu, Babati


maipacarusha20@gmail.com


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amezindua rasmi wiki ya vijana kitaifa kwenye viwanja vya stendi ya zamani mjini Babati Mkoani Manyara.


Waziri Mhagama amezindua wiki hiyo akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuzindua muongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Manyara.


Akizungumza kwenye uzinduzi huo Waziri Mhagama amesema vijana wana uwezo mkubwa wa kufanya vitu tofauti hivyo wapewe nafasi.


Amesema vijana wasiachwe wenyewe ila wasaidiwe katika kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kwani Taifa linawategemea 


Amesema muongozo uliozinduliwa unaelezea kwa kina fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo mkoani Manyara na dira ya mkoa kwenye eneo la uwekezaji na maendeleo.


"Nawashukuru timu nzima ya mkoa wa Manyara kwa kazi nzuri na kubwa tulioshirikiana kwenye uzinduzi wa jarida hili, tunaweka mazingira rafiki kwa kila atakayetaka kuwekeza, tumeanza kutangaza fursa hizi kwa vijana wetu waliofurika mjini Babati kutoka pande zote za Tanzania," amesema.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi Vijana na watu wenye ulemavu, Prof Joyce Ndalichako amesema maadhimisho ya wiki ya vijana yalianza mwaka 2000 ili kuendeleza uzalendo wa waasisi wa nchi.


Prof Ndalichako amesema wataendelea kuwawezesha vijana mikopo inayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuwanyanyua kiuchumi.


Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga amesema wapo kwenye mwezi wa Oktoba ya kibabe hivyo wamejipanga kuhakikisha wanashiriki ipasavyo kwenye maadhimisho hayo.


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul amesema wakazi wa mjini Babati wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyowaletea maendeleo mbalimbali kupitia miradi.


Mbunge wa jimbo la Kiteto, Edward Ole Lekaita amesema wananchi wa Kiteto wanamuombea afya njema, uzima Rais Samia na wanasubiri ifikapo mwaka 2025 wampe kura nyingi za ndiyo kutokana na maendeleo aliyoyafanya.



No comments: