Amani Lengume na Rapasyo Lengume ambapo mifugo yao 220 imetaifishwa |
*Kaya 17 zenye watoto 107 zawa masikini.*
Johnson Laizer, Loliondo
maipacarusha20@gmail.com
Wananchi wa Tarafa ya Loliondo wameiomba Serikali kuunda Tume ya kuchunguza tukio la kutaifishwa Mifugo yao 806 katika tuhuma za kuingizwa kufuata malisho ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti .
Mifugo hiyo, ilikamatwa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti Octoba 26 na baadae kupigwa mnada Octoba 30 katika mazingira yenye utata.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mondorosi juzi wananchi hao wameeleza serikali inapaswa kuchunguza tukio hilo kwani pia Ng'ombe waliokamatwa ni 1036 na sio 806.
Mgogoro wa Mifugo ya wananchi hao kutaifishwa pia liliwasilishwa bungeni wiki iliyopita katika hoja binafsi ya Mbunge wa Jimbo la Emmanuel Oleshangay na serikali imeahidi kuendelea kulifatilia.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angela Kairuki alisema bungeni kuwa Mifugo iliyokamatwa iliingizwa ndani ya hifadhi ya Serengeti na taarifa alizopewa taratibu za kisheria zilifanyika Hadi kupigwa mnada Mifugo hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji Cha Mondoros Joshua Makko akizungumza na wananchi KATIKA mkutano huo |
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Joshua Makko alisema kilichofanywa na askari ni dhuluma kubwa kwa wananchi ndio sababu wanataka uchunguzi ufanyike.
Alisema katika Kijiji chake Kaya 17 zenye watoto 107 zimefilisiwa kwa kunyang'anywa mifugo 220.
" Tunaomba uchunguzi kabisa kwanza Ng'ombe hazikuwa 806 zilikuwa 1036 tunajua waliuza siku Moja kabla ya mnada lakini pia Ng'ombe, mbuzi na Kondoo zilikamatwa nje ya hifadhi "alisema.
Alisema Sasa Kaya zilizotaifishiwa Mifugo zimegeuka masikini.
"Baada ya mifugo kukamatwa Mimi pamoja na Madiwani wawili na wenyeviti wa vijiji vya jirani baada ya mifugo kukamatwa tulikwenda kuomba iachiwe kwani ilikuwa inachungwa eneo la Olkimbai nje ya hifadhi na tupo tayari kwa mazungumzo wakanipa namba zao lakini walitusunbua hadi kuuza mifugo"amesema
Amesema kawaida Ng'ombe zikikamatwa hupelekwa kesi wilaya ya Serengeti lakini safari hii walipeleka kesi Musoma ili tusijuwe zilipo.
"Tuliuliza kesi ipo Mahakama ipo hawajajibu tulienda Muhimu Serengeti lakini baadae tulipata taarifa wameenda Musoma tulikuta tayari wametoa Hukumu eti Ng'ombe zilikuwa Hazina wenyewe na wanapiga mnada"alisema
Alisema walifanikiwa kupata zuio la Mahakama lakini halikuweza kuzuia Mifugo yao kutouzwa
Amani Ole Lengume alisema Ng'ombe wake 220 wametaifishwa walikuwa na uwezo wa kusomesha watoto, kula na kulipa ada za shule lakini sasa hawawezi Tena.
"Tumegeuka masikini, hatuna tena Mifugo, wamechukuwa Mifugo yote, hatuna tena maziwa na sisi Mifugo ndio tegemeo letu alisema huku akilia kwa uchungu.
Rapasyo Lengume amesema wanamuomba Rais Samia kuwasaidia kupata Mifugo yao kwani maisha yao yamekuwa magumu sana.
Nori Kishini mkazi wa kijiji hicho akizungumza katika mkutano huo |
Nori Kishini mkazi wa jiji hicho, alisema serikali inapaswa kuingilia kati ili kuokoa maisha yao kwani wanafilisiwa kinyume cha sheria.
Kishini alisema wanaimani kubwa na serikali ya CCM na Rais Samia kuwa wataingilia kati na kumaliza mgogoro huo.
"Sisi wote ni CCM tunaipenda serikali na tulichagua CCM hivyo sisi Wafugaji tunagombanishwa chama chetu"alisema
Mchungaji Nikolaus Makoo akizungumza katika mkutano huo |
Mchungaji wa Kanisa la Pentecost Soitambu, Nikolaus Mako alisema serikali inapaswa kumaliza mgogoro na kusaidia Kaya zilizopokonywa Mifugo.
"Hizi familia 17 zilizopokonywa Mifugo 220 nazifamu zinatemea Mifugo tu Sasa baada ya kuuzwa Mifugo yao zimekuwa masikini naomba serikali kuingilia kati jambo hili na kurejesha mahusiano mazuri baina ya Jamii na wahifadhi"alisema.
No comments:
Post a Comment