Na Elinipa Lupembe, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (MB), amekagua, Maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusafirisha Umeme cha Lemuguru, Kijiji cha Lemuguru kata ya Matevesi wilaya ya Arumeru, mkaoni Arusha, leo tarehe 26 Novemba, 2023.
Mratibu na Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupozea Umeme Lemuguru, Mhandisi Peter Kigadye, ameeeleza kuwa, utekelezaji wa miradi ya njia Kuu ya umeme, wenye Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Singida mpaka Namanga kuelekea Kenya.
Ameweka wazi kuwa, kufuatia mpango wa Serikali wa maendeleo ya Nishati, imekusudia kuunganisha gridi ya Taifa pamoja na gridi ya nchi za Kenya na Zambia, ambayo itaiwezesha Tanzania kununua, kuuza na kusafirisha umeme wa bei nafuu, unaozalishwa kwa kutumia maji kutoka Ethiopia na kutoka Bwawa la Mwalimu Julias Nyerere.
Mradi wa Kuunganisha umeme Kenya na Tanzania, una umuhimu katika kuwezesha kuunganisha umeme ukanda wa Kaskazini na Kusini kupitia biashara ya Nishati, kwa lengo la kupanua uwezo wa Tanzania na kuunganisha umeme kwa pamoja kwa Afrika Mashariki.
Mradi huo utachangia kuimarisha uwezo wa kusambaza umeme katika nchi zote mbili na eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla na kupunguza gharama za uzalishaji wa umeme, ambao utapunguza gharama za uzalishaji kwa kutumia mafuta mazito na gesi kwa kutumia umeme wa maji, ambao, utapunguza uzalishaji wa hewa ukaa.
Mradi huo wa Kituo cha umeme Lemuguru, umetekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 14.2 na unategemea kukamilika tarehe 28 Februari, 2024 ulihusisha ujenzi wa njia 8 na kusambaza umeme wa Kilovoti 33 zenye urefu wa Kilomita 208 na kupeleka umeme maeneo ya wilaya ya Longido, Monduli, Arumeru na Jiji la Arusha.
No comments:
Post a Comment