JOWUTA kushirikiana vyama vya waandishi Afrika Mashariki kuboresha mazingira ya kazi kwa Wanahabari. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 25 December 2023

JOWUTA kushirikiana vyama vya waandishi Afrika Mashariki kuboresha mazingira ya kazi kwa Wanahabari.

 

Baadhi ya waandishi Toka Nchi za Tanzania na Kenya wakiwa katika picha ya pamoja

Mwenyekiti mpya KCA akipongezwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda William Aloo





Mwandishi wetu, Nairobi


maipacarusha20@gmail.com


Chama cha Wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) kimeahidi kushirikiana na vyama vya wanahabari katika nchi za Afrika Mashariki kuboresha mazingira ya kazi kwa wanahabari.


Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa, Mussa Juma alitoa ahadi hiyo katika mkutano wa Taasisi za waandishi wa habari na Asasi za kiraia ulioandaliwa na chama cha waandishi wa habari wa kujitegemea nchini Kenya(KCA) kujenga mahusiano baina ya vyombo vya habari na Asasi za kiraia.


Juma alisema, kupitia Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, JOWUTA itashirikiana na wanahabari nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuhakikisha mazingira ya kazi kwa wanahabari yanakuwa bora ikiwepo kuvutia uwekezaji zaidi.


"Mazingira ya kazi kwa waandishi wa Afrika ya Mashariki yanafanana hivyo ni muhimu kuendelea kuboreshwa mazingira ya kazi lakini kuomba kufunguliwa fursa kwa wawekezaji sekta ya Habari"alisema

Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa Mussa Juma akiwa katika mkutano huo jijini Nairobi

Alisema Serikali ya Tanzania ipo katika hatua mbalimbali za kuboresha sheria za habari lakini pia imeanza kufanyia kazi suala la uchumi katika vyombo vya habari lengo likiwa ni kuondoa changamoto.


Mwenyekiti wa KCA William Oloo Janak, alisema kuna umuhimu kuwepo kwa ushirikiano kwa waandishi wa Afrika ya Mashariki katika kuboresha mazingira ya kazi.


"Changamoto zetu zinafanana na kuna  jumuiya ya Afrika ya Mashariki inaweza kutuunganisha"amesema


Aloo alitaka kuwepo ushirikiano baina ya asasi za kiraia na vyombo vya habari kwani wote jukumu lao ni moja kusaidia jamii.


Katika mkutano huo, KAC, Chama cha wafanyakazi 

Katika vyombo vya habari Kenya, Jukwaa la wahariri Kenya na Viongozi wa Asasi za kiraia  walikubaliana kushirikiana kutatua changamoto  katika kila sekta zao.

 

Wakati huo huo, Chama cha waandishi wa habari kujitegemea Kenya kimepata viongozi wapya ambapo Araka Matara alichaguliwa kuwa mwenyekiti baada ya Janak kuomba kupumzika.


Makamu Mwenyekiti alichaguliwa Irine Nasimiyu alichaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti na John Shilitsa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu.


Katika uchaguzi huo, Bernard Kwalia alichaguliwa tena kuwa Mweka hazina wa chama hicho.


Akizungumza baada ya kuchaguliwa Matara alimuomba Aloo kuendelea kuwa mshauri wa chama na alipongeza JOWUTA na APC kushiriki mkutano huo.


"Nashukuru wenzetu Tanzania kuja kutuunga mkono na tunaahidi mwakani tutakuja Tanzania kujifunza zaidi.


Katika Mkutano huo pia viongozi wa chama cha wandishi habari mkoa Arusha (APC) walishiriki akiwepo Katibu Mkuu Zulfa Mfinanga na Mjumbe wa kamati ya Utendaji Pamela Mollel.

Baadhi ya waandishi wakifuatilia mkutano huo


No comments: