RC MONGELLA : WALIMU SIMAMIENI UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU NA VIFAA VYA SHULE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 28 December 2023

RC MONGELLA : WALIMU SIMAMIENI UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU NA VIFAA VYA SHULE

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akiwapa maelekezo Viongozi wa wilaya ya Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akimpa maelekezo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini


Na: Elinipa Lupembe, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amewagiza walimu wote mkoa wa Arusha, kusimamia utunzaji wa miundombinu yote inayojengwa pamoja na vifaa vyote vinavyowekezwa kwenye shule zao.


Agizo hilo limekuja wakati Mhe. Mongella, akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule, ikiwa ni maandalizi ya mapokezi wanafunzi, muhula wa masomo unaotarajia kuanza, Januari 2023, na kukerwa kwa baadhi ya majengo na vifaa kuanza kuharibika kutokana na uangalizi mbovu.


Mhe. Mongella amewaagiza walimu wote mkoani humo, kusimamia utunzaji wa majengo na vifaa vyote vya shule, ikiwa ni pamoja na kutumia asilimilia 35 ya fungu la ukarabati kupitia fedha za uendeshaji wa shule, kufanya matengenezo madogo madogo pindi unapotokea uharibifu.


"Tunzeni majengo haya, Serikali imetumia fedha nyingi kuyajenga, kuweni wazalendo,  wasimamieni na wajengeeni uwezo wanafunzi kuthamini na kutunza vifaa vya shule, majengo haya yanapaswa kutumika sasa na vizazi vijavyo, jukumu la kusimamia utunzaji ni lenu walimu, hakuna namna ya kukwepa". Amesisitiza Mhe. Mongella.


Aidha, amewasisitiza kutambua  nia ya Serikali ya kuwekeza fedha nyingi, ni kuhakikisha mazingira ya kujifunza na kufundisha kwa  walimu na wanafunzi, yanakuwa bora na rafiki, hivyo walimu na wanafunzi wanalo jukumu la kutunza vifaa vyote vya shule.



Ameongeza kuwa, licha ya kuwa, idadi ya wanafunzi ni kubwa, amewataka wakuu wa shule, kuweka utaratibu wa kugawa majukumu ya usimamizi wa vifaa vya shule, kupitia walimu wa madarasa, kila mwalimu awe na eneo lake dogo la usimamizi, likiratibiwa na walimu wa vifaa na mazingira shuleni.


"Mwalimu mkuu, ni mkuu wa Taasisi mali na watumishi, endapo atashindwa kusimamia majukumu yake inamaanisha hatoshei kwenye nafasi hiyo, ninawaagiza Wakuu wote wa shule, kusimamia utunzaji wa mali za shule, kazi ya Mkuu wa shule ni kusimamia taaluma pamoja na vitendea kazi vyote vinavyosaidia kuimarisha na kufikia maelengo ya kitaaluma" Ameagiza Mhe. Mongella

No comments: