SIMANZI WILAYANI HANNANG' WATU 23 WAFARIKI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 3 December 2023

SIMANZI WILAYANI HANNANG' WATU 23 WAFARIKI






Na: Mwandishi Wetu, Hannang'


maipacarusha20@gmail.com


Takribani watu 23 wamebainika wamekufa kutokana na mafuriko ya Maji ya  aina yake ambayo yamesababishwa na kuporomoka kwa mlima Hanang, wilayani Hanang mkoani Manyara.


Mafuriko hayo yametokana na mvua ambayo ilianza kunyesha Jana majira ya saa tatu usiku na kuendelea hadi leo asubuhi.


Mkuu wa wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amesema leo Desemba 3, 2023 kuwa hadi mchana miili ya watu 23 imepatikana na imepelekwa hospital ya Tumaini ya mjini Katesh.


Amesema pia kuna majeruhi zaidi ya 70 ambao tayari wamefikishwa hospital ya wilaya hiyo ya Tumaini.


"Uokowaji unaendelea katika maeneo ya Katesh na Gendabi ambapo mafuriko hayo yamepita na kusomba nyumba kadhaa, maeneo ya biashara na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Katesh"amesema


Amesema uokoaji unaendelea kufukua tope ambalo limefunika nyumba, maduka na maeneo mbalimbali.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hanang, Rose Kamili amesema zoezi la uokoaji bado ni gumu kwani kuna maeneo mengi hayafikiki.


Amesema katika maeneo hayo ya mlima ambapo Kuna mabonde na vyanzo vya maji bado kuna Maji yanatoka juu ya Mlima na kurudi chini.


"Mimi nipo eneo la tukio hali sio nzuri kuzunguka mlima Hanang na tunaendelea na zoezi la uokoaji"amesema


Jeremiah Siay mkazi wa Katesh amesema ndugu zake wawili  anahofu wamesombwa na mafuriko kwani hawajulikani walipo.


"Tunahangaika kuwatafuta ndugu zangu ma majirani hali sio nzuri mlima umepasuka na kuanza kushusha Maji chini"amesema.


Amesema mafuriko hayo kutoka mlima yamevunja majumba,kuchukuwa Mifugo na kuharibu mali nyingi.


Mkuu wa mkoa wa Manyara, Qeen Sindika na ujumbe wake waliokuwa Wilayani Kiteto kikazi wapo njiani kwenda wilayani Hanang


No comments: