Na:Andrea Ngobole, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Kamishna wa fedha na maendeleo kutoka wizara ya fedha Nchini Dkt. Charles Mwamaja ameutaka uongozi wa chuo kikuu Mzumbe kubuni njia mbadala ya kupata mikopo kwa wajasiriamali wadogo kupitia mfumo wa mikopo kutoka kwa watu wengi kwa njia ya mtandao.
Ameyasema hayo jijini Arusha katika kongamano la kimataifa la wajasiriamali wanaonufaika na mikopo kutoka kwa watu wengi iliyoasisiwa na chuo kikuu mzumbe kwa kushirikiana na sido kwa udhamini wa shirika la kimataifa la maendeleo la kanada (DANIDA) ambapo jumla ya wajasiriamlai mia moja wameweza kupata mikopo ya kuanzisha na kuendeleza biashara katika mikoa ya Arusha, Tanga, Daresalaam, Morogoro na Mbeya.
Kamishna Mwamaja Amesema serikali inaamini nafasi ya kijana katika kuwaendeleza na kutengeneza mazingira wezeshi ili kujikwamua kiuchumi na kutengeneza ajira kupitia biashara wanazoanzisha hivyo fursa ya mikopo isiyohitaji dhamana isiyohamishika ni muhimu na chachu ya maendeleo ya Taifa.
Amewataka wataalamu wa Biashara na mikopo jumuishi kutoa matokeo ya tafiti wanazozifanya badala ya kuzifungia makabatini ili zijulikane kwa watu wengi na kufanya biashara kuwa pana zaidi kwa chachu na maenedeleo ya taifa kwa ujumla.
"Mikopo hii isiyokuwa na dhamana na riba nafuu haina kikwazo kwa mkopaji na ni njia bora zaidi ya kuongeza kipato kwa watu wengi hususani vijana kwani kwa utafiti uliofanywa unaonesha wamiliki wa nyumba nchini Tanzania hawazidi asilimia kumi hivyo kusaidia kuondoa vikwazo kwa waajasiriamali wadogo." Alisema kamishna Mwamaja
Awali akimakaribisha Kamishna Mwamaja, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha amesema kuwa wanajivunia kuja na matokeo ya utafiti huo uliowezesha wajasiriamali wadogo kupata mikopo Kwa urahisi kupitia majukwaa ya mtandaoni baada ya kuweka wazo linalowavitia watu wengi kikuchangia mtaji wa mkopo na Kisha kurejesha Kwa wakati.
Amesema mradi huo umewezesha wajasiriamali 187 kupata mafunzo ya jinsi ya kuomba mikopo mtandaoni na Kwa kiwango kikubwa wameshaanza kupata mikopo hiyo.
Mratibu wa mradi huo Dkt. Nsubili Isaga Akitoa matokeo ya mradi huo amesema kuwa utafiti huo umeenda moja Kwa moja kuwakwamua vijana wengi kuanzisha Biashara na kupata mikopo rafiki Toka Kwa mitaji halaiki isiyohitaji dhamana ya vitu visivyohamishika.
Amewashauri vijana wengi wahakikishe wanashirikiana na Sido ili walelewe vema kupata sifa stahiki za kukopesheka.
Naye moja wa wanufaika wa mradi huo Toka mkoani Tanga Agness Mwamanga amesema mradi huo umemuwezesha kuanzia na mkopo wa shilingi laki tatu ambazo zimemsaidia kuendeleza Biashara yake ya ufumaji wa masweta ya watoto ambayo aliuza na kumuwezesha kurejesha mkopo Kwa wakati na kujipatia faida ya shilingi laki Tano Kwa muda wa miezi miwili tu.
Amewashukuru Sido na Chuo Kikuu Mzumbe Kwa mafunzo ya andiko la mradi linaloeleweka na likiwekwa katika jukwaa la mtaji jumuishi ni rahusi kupata kuchangiwa mtaji wa Biashara Yako kwani inaonesha uhalisia.
No comments:
Post a Comment