Fred Lowassa awaliza waombelezaji mazishi ya Lowassa - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 17 February 2024

Fred Lowassa awaliza waombelezaji mazishi ya Lowassa

 




Mussa Juma,MAIPAC

maipacarusha20@gmail.com


Hutuba ya shukrani ya Fred  Lowassa Mtoto wa kwanza wa Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa Leo imewaliza mamia ya watu walijitokeza katika mazishi.


Akizungumza kwa  utulivu, Fred Lowassa ameelezea Mapito ya Baba yake Edward Lowassa tangu alipoanza kuumwa hadi mauti yake.


Fred Lowassa alimshukuru sana Rais wa Jamuhuri wa Muungano, Samia Suluhu Hassan  kwa mchango mkubwa wa kuokoa maisha ya baba Yao.


Amesema mara tu baada ya baba yake kuzidiwa baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospital ya Muhimbili, Rais Samia alitoa fedha zake binafsi kugharamia matibabu kwenda Afrika kusini wakati michakato mengine ya Serikali ikiendelea.


"Mama ulifanya haya sio kwa sababu  wewe ni  Rais hapana umefanya kwa sababu wewe umekuwa mlezi wa familia ,umekuwa ukimpigia mama simu mara kwa mara kujua hali ya baba na kumtia moyo"amesema


Fred amesema yeye binafsi na familia wanakosa maneno yanayotosha kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa mchango mkubwa aliyotoa kupigania afya ya baba Yao.


Fred pia alimshukuru sana Mama yake, Regina Lowassa kwa moyo wake wa ucha Mungu.

Amesema mama yake Regina tangu baba yake, ameanza kuumwa amekuwa akikesha kumsaidia kuokoa maisha yake.


"Mama ulikuwa ukikesha usiku na mchana kumsaidia Baba ...kuna siku tulikuwa na Shangazi akawa anasema sijuwi tutakulipa nini kwa jinsi ambavyo ulikuwa unajitolea kuokoa maisha ya Baba"amesema


Fred pia alimshukuru Aliyekuwa msaidizi binafsi ya Lowassa, Daniel Porokwa kwa kazi kubwa aliyokuwa anafanya kuokoa maisha ya baba yao.


Amesema pia wanawashukuru sana waliokuwa  walinzi wa Lowassa kwani kwa miaka mitatu ya ugonjwa wamekuwa nae wakilala pamoja kumsaidia.


Fred lowassa pia aliwashukuru sana waombolezaji, wakiwepo ,Wabunge, viongozi, kutoka nchini Kenya wa jamii ya kimasai waliofika katika mazishi.


Amesema Lowassa, alikuwa Laigwanani wa Afrika ya Mashariki na aliweza kuwaunganisha jamii ya kimasai kutetea jamii hiyo ikiwepo suala la ardhi.

###


No comments: