TIA KUANZA MFUMO MPYA KUSOMA KIMTANDAO NJE YA VITUO VYAO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 29 February 2024

TIA KUANZA MFUMO MPYA KUSOMA KIMTANDAO NJE YA VITUO VYAO

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) inatarajia kuanza mfumo mpya wa kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa mtandaoni nje ya vituo vyao vya masomo tofauti na sasa ambapo mwanafunzi hulazimika kuwepo katika kituo cheke cha masomo.

 

Hayo yamebainishwa mkoani Morogoro na mratibu wa Tathimini na ufuatiliaji wa mradi wa mageuzi ya kiuchumi kwa vyuo vya elimu ya juu (HEET) Magreth Emanuel wakati wa mafunzo kwa wakufunzi kutoka taasisi hiyo ya uhasibu Tanzania (TIA).


Mradi huo umelenga kuwafikishia wanafunzi vitu vya kusoma kupitia mtandao kwenye maeneo watakayokuwepo.


Aidha mratibu huyo amesema kuwa Mfumo huu mpya ni mapinduzi makubwa katika taasisi ya uhasibu Tanzania ambao utawasaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya usomaji wa masomo mtandaoni.


"Mfumo huu umeletwa kupitia mradi huo wa HEET ili kuhakikisha unaboresha maeneo mbalimbali katika taasisi hii," amesema Mratibu huyo.


Kwa upande wake mkuu wa chuo TIA profesa William  Pallangyo amesema mradi huo wa HEET umeelekeza kuhakikisha katika kipindi hiki ambacho mitaala ya chuo inaisha muda wake, miitaala mipya inatakiwa kuwa ya kimataifa zaidi.


Pallangyo amesema kuwa uandaaji wa material hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa mageuzi ya kiuchumi Kwa vyuo vya elimu ya juu  HEET ambao unalenga kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia Katika taasisi ya elimu ya juu.


Hata hivyo amesema TIA ni mojawapo wa wanufaika wa mradi huo hususani kwenye eneo la mitaala, miundombinu, Tehama na kujenga uwezo wa watumishi.


Pallangiyo pia amesema online learning material zinazokusudiwa kuandaliwa zitawasaidia  wahadhili kufundishia na kufanya tathmini kidigitali ambapo wanachuo watapata fursa ya kujifunza wakati wowote wakiwa Mahalia popote kupitia teknolojia hiyo.


Wakufunzi kutoka taasisi ya  Uhasibu Tanzania (TIA) wamesema mradi huo wa HEET utasaidia wanafunzi kupata huduma bora za kujisomea pamoja kuhakikisha kunakuwa na kipato endelevu kwa mtu mmojammoja  na kukuza kipata katika taasisi ya uhasibu Tanzania.


Aidha walisema kuwa mradi huo pia utarahisisha kazi nzima ya ufundishaji ambapo utaweza kufanya kazi hata kama uko nje ya kituo chako Cha kazi.


No comments: