MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AVUTIWA NA UTENDAJI WA TANAPA, KUTEMBELEA HIFADHI YA SERENGETI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 7 March 2024

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AVUTIWA NA UTENDAJI WA TANAPA, KUTEMBELEA HIFADHI YA SERENGETI



Mkurugenzi wa idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Mobhare Matinyi akiwa katika kikao na menejimentinya Tanapa 




Na Mwandishi wetu, MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


Mkurugenzi wa idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Mobhare Matinyi, ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kukutana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Mussa Juma Kuji, na kisha kufanya kikao kifupi na Menejimenti ya TANAPA jijini, Arusha

Katika kikao hicho alipewa maelezo ya utendaji kazi wa Hifadhi zote nchini ambapo naye amesema atafanya ziara ya siku tatu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Bw. Mobhare Matinyi katika Ziara hiyo ya siku 3 kutembelea Hifadhi za Taifa na kujionea shughuli za Utalii na Uhifadhi na kukagua miundombinu hasa barabara katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Kamishna wa uhifadhi Tanapa Mussa Juma Kuji akimkabidhi MSEMAJI wa Serikali Jarida la Tanapa




No comments: