Na: Lilian Kasenene,Same
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amewaagiza maafisa ardhi wa ngazi zote za wilaya mkoani humo kutotoa hati miliki za viwanja kabla ya mwenye kiwanja kupanda miti kuanzia mitano ili kuhamasisha shughuli za upandaji miti na utunzaji wa mazingira ili kuufanya mkoa huo kuwa wa kijani.
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo katika Uwanja vya shule ya sekondari Same wakati akizungumza na wananchi kuelekea maadhimisho ya siku ya Misitu Duniani na siku ya upandaji miti kitaifa yanayoadhimishwa katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dk Philip Isdor Mpango.
“Hakuna mtu kukata mti hata kama ni wa kwake, tunakuruhusu upande mti ni wa kwako lakini ukitaka kuukata lazima tukubaliane unaukata uko wapi au kwa shughuli gani, lakini ndugu zangu wa Same tunakwenda kulima kandokando ya nvyanzo vya maji,ndio maana kipindi cha mwaka huu kilichopita tumepoteza watoto wetu wengi wa shule za sekondari na msingi kwa sababu nyumba kujengwa chini hivyo mvua zilizonyesha zimeporomosha magema na kuangusha nyumba,”amesema.
Babu amesema hali ya wilaya ya same kwa sasa si ya kuridhisha hivyo wamehamua kuifamya maadhimisho hayo wilayani humo kwa sababu ya muonekano wake kutukowa nzuri ni kutokana na ukame, na ili kuirejesha kwenye ukijani, kupanda miti ya kutosha, kurudisha same ya kijana na kutekeleza agizo ya vikao vya ushauri vya mkoa .
“Dhamila ya mkoa wa Kilimanjaro ni kuirudisha kwenye ukijani na kuwa katika hali yake ya zamami, miti tuliyoikuta ni ya zamami iliyopandwa na babu zetu mingine imechoka na kuanguka na kuwa na upungufu wa miti,” amesema .
Amesema kumekuwa na watu wasiopenda maendeleo wao wamekuwa na kazi ya kukata miti ovyo kwenye vyanzo vya maji na kukata miti kwenye milima na kuharibu mazingira na wamekuwa wakifanya kazi hizo usiku.
Mkuu huyo wa Mkoa akaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamaia wafugaji, na kutaifisha mifugo mbuzi na ng’ombe na kuwa mari ya serikali ili miti ieshimiwe na kwamba nusu ya miti inayopandwa imekuwa ikiliwa na mifugo.
“Mfano eneo la Chekereni miti zaidi ya elfu saba iliyopandwa nusu yake imeliwa na Ng’ombe, hatuwezi kufanyakazi ya kupanda na watu wanaleta mifugo, tukumbuke misitu ina mchango mkubwa, na inachangia asilimia tatu ya pato la taifa,”amesema.
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni, akazungumzia hatua walizochukua kama wilaya kwenye upandaji wa miti ambapo amesema katika kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa wilaya imekuwa ikipanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yameikumba nchi huku wakitekeleza maagizo ya Rais samia Suluhu Hassan.
Mgeni amesema wilaya Same mpaka sasa miti zaidi ya laki tano (500,000) imepandwa kandokando ya barabara kuanzia mwanzo wa wilaya mpaka mwisho na hiyo ni katika kuuwisha kampeni ya Fanya Same kuwa ya Kijani na hali ya hewa imeanza kubadilika ikiwemo kunyesha kwa mvua mara kwa mara.
Akimwakilisha katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,kaimu mkurugenzi wa idara ya misitu na nyuki kutoka wizara hiyo,Daniel Pangras,akizungumzia umuhimu wa maadhimisho hayo yenye kauli mbiu, "misitu na ubunifu" amesema lengo kuu la maadhimisho hayo Mwaka huu ni kutoa Elimu kwa wananchi na kutambua mchango wa Serikali katika suala zima la Misitu na upandaji miti.
Aidha Panglas amesema misitu ina umuhimu kijamii, kiuchumi, kimazingira na ajira.
“Iko dhana ya watu kupanda miti lakini sisi kama watanzania na wataalamu tumekuwa tukiishia kwenye elimu ya kupanda miti na sio kutunza miti lakini kupitia mkusanyako huu wataalamu watafanya kazi ya kufundisha namna boira ya kupanda na kutunza miti,”amesema.
Maadhimisho ya siku ya Misitu Duniani na siku ya upandaji miti kitaifa yanafanyika wilayani Same mkoani Kilimanjaro huku makundi na wadau mbalimbali wa masuala ya Misitu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro wamejitokeza katika kuadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment