Na: Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
MKUU wa Wilaya Kilombero Dunstan Kyobya amewataka wananchi wilayani humo kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na mvua inayoendelea kunyesha na kusabababisha mafuriko, kwa kuwasimamia watoto kutokwenda kucheza kwenye madimbwi.
Alisema hayo wakati akikagua na kutoa msaada kwa abiria zaidi ya 500 waliopata changamoto ya kunasa eneo la Lumumwe wilayani humo baada ya mvua zinazoendelea kunyesha kuharibu Miundombinu ya Madaraja na Makaravati na kusababisha kifusi kufunika Reli ya TAZARA .
"Msiwaache watoto wakaenda kucheza kwenye madimbi ya maji ni hatari wanaweza kuzama na kupoteza maisha" alisema.
Aidha, aliwajulisha abiria sasa treni iliyokuwa inafanya safari zake ndani ya Dar Esa Salam kwa jina Maarufu Mwakyembe, imefika Mlimba na itaanza safari ya kuelekea Jijini Dar es Salaam .
Pia aliwaambia wananchi wa kata ya Kalengakelu kuwa wakala wa barabara Tanzania (Tanroads ) wataanza kufanya kazi ya kuunganisha barabara katika maeneo yaliyokatika katika vijiji hivyo.
Abiria hao waliokuwa wanasafiri kutoka Makambako kuelekea Kidatu wilayani Kilombero, kwa kutumia usafiri wa treni kushindwa kupita maeneo hayo kutokana na kuangukiwa kifusi katika barabara hiyo.
Kwa mujibu wa mhandisi wa treni hiyo Kelvin Kyara alisema kuanzia sasa safari zitaanzia Mlimba mjini wilayani humo hadi Dar es Salaam kwa kutumia tren ya mwakyembe na kusitisha safari za Mkambako.
Alisema miundombinu ya tren imeharibika watajitahidi kutengeneza haraka ili watu waendelee kusafiri kama zamani.
No comments:
Post a Comment