DK BITEKO-KUKATIKA KWA UMEME NCHINI SI MGAO NI HITILAFU ZA HAPA NA PALE ,MAJI YAINGIA KITUO CHA UMEME KIDATU MITAMBO YAJIZIMA,HUDUMA YA UMEME YAANZA KUREJEA BAADHI YA MAENEO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 2 April 2024

DK BITEKO-KUKATIKA KWA UMEME NCHINI SI MGAO NI HITILAFU ZA HAPA NA PALE ,MAJI YAINGIA KITUO CHA UMEME KIDATU MITAMBO YAJIZIMA,HUDUMA YA UMEME YAANZA KUREJEA BAADHI YA MAENEO

 





Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


NAIBU Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko amesema  kuwa mgao wa umeme kwa sasa umepungua kwa kiwango kikubwa na nchi haina upungufu wa umeme na kinachotokea ni hitilafu za hapa na pale za nguzo kuanguka hasa kipindi hiki cha mvua za mafuriko zinazoendelea kunyesha na kuathiri maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya umeme.


Dk Biteko alisema hayo Aprili 1,2024 alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme la Kidatu,baada ya baadhi ya mitambo ya kuzalisha umeme kujaa maji na kujizima yenyewe ili kujilinda kutokana na mfumo wake ulivyo.


Aliwatoa wasiwasi watanzania kutokana na changamoto iliyojitokeza usiku wa kuamkia Aprili mosi 2024 ya itilafu ya kukakatika kwa umeme karibu nchi mzima kutokana namaji hayo kuingia kwenye mitambo, lakini kutokana na juhudi zilizofanywa na wataalamu wa shirika la umeme Tanzania(TANESCO) ambapo walifanikisha kuyaondoa maji..


"Mfumo wa mitambo iliyopo Ina mfumo wa kujilinda, ambapo maji yalijaakwa wingi na kusababisha mitambo kujizima,lakini wataalamu wetu wa Tanesco wamefanya kazi usiku kucha kwa kuyaondoa maji hayo, na walifanya kazi nyingine ya kufungua mitambo na kuisafisha na kuweka oil mpya na kuiwasha,na sehemu kubwa ya nchi yetu umeme umerejea,"alisema.


Naibu Waziri mkuu huyo alisema mashine tatu ziko kwenye hali nzuri ya kuendelea kuzalisha umeme, na kwamba bado kuna mashine mmoja inakamilishwa kutengenezwa ili kurudi katika hali ya kawaida ya kiwango Cha uzalishaji wa umeme wa kituo hicho.


Aidha aliwatoa wasiwasi watanzania kuwa changamoto iliyotokea ni kwa sababu ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.


"Niwatie wasisi watanzania na niwaahidi kuwa Shirika letu la umeme linafanya Kila liwezalo kuhakikisha kwamba kila mtanzania ambaye ni mteja wetu anapata umeme bila matatizo, na ametoa pole kwa usumbufu waliopata Toka usiku hadi mchana huu tulipoanza kurejesha umeme taratibu nchini,"alisema.


Pia alisema jambo hilo la kukatika kwa umeme hakukuwa la kusababishwabna mgao Bali limesababishwa na maji yaliyoingia kwenye jengo la mitambo ya kuzalisha umeme.


Alisema kwamba kutokana na utabiri wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) mvua kuendelea kunyesha kwa wingi wizara na Tanesco zinaendelea kuchukua kila aina ya tahadhari ili kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.


Alitolea mfano kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere(JNNPH) kuwa mashine moja inayozalisha umeme lakini wataalamu walikadiria kujaa maji Desemba Mwaka 2026 lakini ndani ya msimu huu limekaribia kujaa na tahadhari zimeshatolewa.


Naibu Waziri Mkuu huyo alisema majanga hayo ya mvua za el nino na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba wamekuwa wakiomba madhara ya mvua hizi yasiwe makubwa na kusababisha hasara za kiuchumi na watu kupoteza maisha kutokana na mafuriko yanayoweza tokea.


Dk Biteko akizungumzia athari za mvua zinazoendelea kunyesha mwaka huu, alisema hakuna sekta iliyobaki Salama ambapo alitolea mfano namna zilivyoathiri miundombinu ya barabara.


Mkurugenzi wa Tanesco Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga aliwaomba radhi watanzania kwa namna kazi na shughuli zao kusimama huku akimmshukuru Naibu Waziri Mkuu kufika kituoni hapo ambapo aliwapongeza wafanyakazi wa Tanesco kwa kuelendelea kufanyakazi kwa bidii na kujituma.


Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Morogoro, mkuu wa Wilaya ya Kilombelo Dunstan Kyobya aliwasisitiza wananchi wanaoishi mabondeni kuhama haraka kutokana na mvua zinazosababisha mafuriko na kumuhakikisha Naibu Waziri Mkuu kuwa maeneo ya nyanzo vya maji kuendelea kulindwa.


No comments: